BARAZA LA ARDHI LA NYUMBA


 Utangulizi
Sheria ya Ardhi Na. 4 na Sheria ya Ardhi ya vijiji Na. 5 za mwaka 1999 zimetungwa ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kutekeleza Sera yaTaifa ya Ardhi ya mwaka 1995. Sheria hizi zinaainisha vyombo pekee vya kushugulikia migogoro ya ardhi na nyumba.Vyombo hivyo ambavyo ni mahakama kwa mujibu wa sheria hizi ni:-
(i)   Baraza la Ardhi la kijiji - (The Village Land Council).
(ii)   Baraza la kata - (The Ward Tribunal),
(iii) Baraza la Ardhi na Nyumba la
Wilaya - (The   District Land
and Housing Tribunal),
(iv) Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi - (The High Court-Land Division),
(v) Mahakama ya Rufaa ya Tanzania- (The Court of Appeal of Tanzania)
Mfumo huu wa utatuzi wa migogoro unaoanzia katika ngazi ya kijiji ni mfumo mpya ambao unalenga kuchukua muda mfupi na kutumia taratibu rahisi na shirikishi zisizokuwa na gharama kubwa kwa watanzania.
 
Sheria Na.2 ya mwaka 2002,The Land Disputes Courts Act, 2002.
 • Imeanza kutumika tarehe 1.10.2003.
 •  Inafuta mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo, Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya kusikiliza na kuamua masuala yote ya madai kuhusu ardhi.
 • Inafuta Mabaraza ya Nyumba ya Mikoa, Baraza la Rufaa la Nyumba, Mabaraza ya Usuluhishi wa Ardhi ya Wilaya/Mikoa na Baraza la Rufaa la Ardhi.
 • Inaunda na inatoa majukumu na mamlaka ya Mahakama zilizotajwa katika Sheria Na.4 na 5 za mwaka 1999 kushugulikia migogoro ya ardhi na nyumba.Baraza lina mamlaka ya
  usuluhishi na endapo wahusika hawaridhiki na uamuzi wake wanaruhusiwa  kupeleka masuala yao kwenye Baraza la Kata.
(ii) Baraza la Kata:
 • Baraza hili ni lile lililoundwa chini ya Sheria Na.7 ya mwaka 1985- The Ward Tribunal Act, 1985. 
 • Baraza hili pamoja na majukumu yake chini ya Sheria Na.7 ya mwaka 1985, limeongezewa mamlaka ya kimahakama ya kushugulikia usuluhishi na maamuzi ya migogoro ya ardhi kwenye eneo lake. 
 • Rufaa kutoka Baraza la kata zinapelekwa kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
MABARAZA
 
(iii) Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
 • Baraza hili linaundwa na Mheshimiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria Na.2 ya mwaka 2002.
 • Kwa mujibu wa sheria, linaweza kuundwa katika ngazi ya wilaya, Mkoa au kanda kutegemeana na wingi wa migogoro ya ardhi na nyumba kwenye eneo husika.
Mtu ambaye hataridhika na uamuzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya atakuwa na haki ya kukata rufaa Mahakama Kuu - Kitengo cha Ardhi. Vivyo hivyo, yule ambaye hataridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu - Kitengo cha Ardhi, atakuwa na haki ya kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.
 
Kazi za Baraza
 • Baraza la Ardhi la kijiji linasuluhisha au linasaidia Wananchi wenye migogoro katika kijiji kufikia muafaka.
 • Baraza la Ardhi la kijiji huitisha kikao baada ya pande zinazohusika kukubali huduma ya upatanishi ya Baraza hilo. Hata hivyo, wananchi hawalazimiki kutumia huduma ya Baraza la Ardhi la kijiji na hata kama watatumia huduma hiyo, wanaweza pia kukataa maamuzi yake. Kwa sababu hiyo, wananchi wanaweza kupeleka masuala yao moja kwa moja kwenye Baraza la Kata.
 • Kazi ya Baraza la kata na Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kimsingi ni kupokea na kusikiliza migogoro ya ardhi na nyumba. Migogoro yote ambayo thamani yake kifedha haizidi milioni tatu (3) huanza kushugulikiwa na Baraza la Kata. Hata hivyo, kama mhusika anawakilishwa na wakili au yapo mazingira mengine maalum, kesi hiyo inaweza kufunguliwa moja kwa moja katika Baraza la Wilaya.
 • Baraza la Wilaya linapokea migogoro yote ambayo thamani ya nyumba, ardhi au kinachodaiwa ni zaidi ya milioni tatu (3) na hakizidi milioni arobaini (40) kwa vitu vinavyohamishika na milioni hamsini   (50) kwa vitu visivyohamishika.
Wajumbe/ Washauri (Assesors) wa Baraza
Mfumo mpya wa utatuzi wa migogoro ya ardhi ni mfumo shirikishi kwa sababu unawashirikisha wananchi katika kutatua migogoro yao, kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mahakama Kuu-Idara ya Ardhi. Wananchi wanashiriki kutokana na baadhi yao kuteuliwa kuwa wajumbe au washauri (assessors) wa Baraza.
 • Kwa mujibu wa Sheria Na.S ya mwaka 1999, Baraza la Ardhi la Kijiji lina wajumbe saba (7) na lazima watatu (3) kati yao wawe wanawake. Wajumbe hao wanateuliwa na Halmashauri ya kijiji na majina yao yanafikishwa kwenye Mkutano Mkuu wa kijiji ili yathibitishwe kabla ya kuanza kazi.
 • Wajumbe wa Baraza la Kata, kwa mujibu wa Sheria Na.7 ya mwaka 1985 (The Ward Tribunal Act, 1985), wanatakiwa wawe kati ya wanne (4) na wanane (8) na kati yao, watatu (3) lazima wawe wanawake.
 • Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, kwa mujibu wa Sheria Na.2 ya mwaka 2002 lina wajumbe wasiozidi saba (7) na watatu (3) kati yao, lazima wawe wanawake. Wajumbe hawa huteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi kutokana na mapendekezo ya Mkuu wa Mkoa na lazima watoke katika eneo la Wilaya husika.
Sifa za Mjumbe
(a) Awe   mtu   mwenye   heshima, mtu   mwenye   msimamo   na ufahamu wa Sheria za Ardhi za eneo husika.
(b)  Lazima awe raia wa nchi hii na mkazi wa Kijiji, Kata au Wilaya husika.
(c)   Umri wake uwe miaka 18 na kuendelea kwa Baraza la Ardhi la Kijiji, na Baraza la Kata na Miaka 21 na kuendelea kwa Baraza la Ardhi   na Nyumba la Wilaya.
(d)   Awe na akili timamu na asiwe
na   kumbukumbu   zozote za makosa ya jinai.
(e)   Asiwe   Mbunge   au   Hakimu katika Wilaya husika, Diwani au mjumbe wa   Halmashauri   ya Wilaya, Kata au Kijiji.
(f)  Kwa    Baraza    la   Ardhi    na Nyumba la Wilaya, kiwango cha chini cha elimu yake kiwe kidato cha nne (4)
7.   Uwakilishi
Mawakili hawaruhusiwi kuwakilisha wananchi katika Baraza la kata isipokuwa katika Baraza laArdhi na Nyumba la Wilaya. Hata hivyo, kama mtu hawezi kufika mbele ya
Baraza la Kata kutokana na sababu za msingi, Baraza linaweza kumruhusu ndugu wa karibu kumwakilisha mtu huyo.
 
8    Utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza
Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya hutekeleza hukumu zake lenyewe kwa kutumia Madalali wake - tribunal Brokers. Vile vile Baraza hili linasimamia utekelezaji wa hukumu za Baraza la Kata . Kwa sababu hiyo. Baraza la Kata halina mamlaka ya kukaza hukumu zake lenyewe.
 
Kwa maoni au maswali
wasiliana na :
Baraza laArdhi na Nyumba
S.LP 2616, Dar es Salaam
Simu: 212009

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni