SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI

1
[SURA ya 322] Sheria ya Jeshi La Polisi Na Huduma Saidizi [Sheria Kuu]
_______
MPANGILIO WA VIFUNGU
______
Kifungu Jina
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA MWANZO
1. Jina fupi na utumikaji
2. Ufafanuzi.




SEHEMU YA PILI
MUUNDO, UTAWALA NA WAJIBU WA JESHI LA POLISI
3. Uanzishwaji wa Jeshi la polisi.
4. Muundo wa Jeshi la Polisi.
5. Wajibu wa Jeshi la Polisi.
6. [Imefutwa.]
7. Mamlaka ya Mrakibu Mkuu
8. Utawala wa Jeshi.
9. Uwakilishi wa Mrakibu Mkuu
10. Maafisa wasimamizi wa kituo cha polisi kutunza vitabu husika na kupeleka marejesho
11. Maafisa wasimamizi wa polisi kuwajibika kwa maghala.
SEHEMU YA TATU
UTEUZI, UANDIKISHWAJI, UTUMISHI NA KUONDOLEWA
12. Uteuzi wa maafisa polisi.
13. Kipindi cha kuwaajiri marakibu
14 Uandikishwaji wa askari polisi, wafualitiliaji na wanafunzi katika Jeshi la Polisi
15. Tangazo la kujiunga na Polisi
16. Masharti ya likizo.
17. Kuajiriwa upya
18. Kuajiriwa upya baada ya kuondolewa
19 Utumishi katika Jeshi la Polisi jingine yaweza kuhesabika kama utumishi katika Polisi
20. Maafisa polisi kutokujiuzulu bila ruhusa.
21. Wanachama wa Jeshi kutokujihusisha na ajira nyingine
22. Kuongeza muda wa utumishi pale panapokuwa na vita
23. Kuondolewa
24. Masharti katika kuhesabu makosa ya utumishi kwa ajili ya kuondolewa.
25. Kuondolewa baada ya kipindi cha utumishi kumalizika
26. Silaha na vifaa vya askari kuwasilishwa vitakapoacha kuwa mali ya Jeshi.
2
SEHEMU YA NNE
MAMLAKA NA WAJIBU WA MAAFISA POLISI
27. Mamlaka ya jumla na wajibu wa maafisa polisi
28. Askari polisi kuchukuliwa kama afisa magereza katika mazingira
fulani.
29. Maafisa polisi wanaweza kutumia silaha katika jambo fulani.
30. Mamlaka ya kuweka habari na malalamiko
31. Dhamana ya polisi
32. Mahudhurio ya shahidi
33. Kumbukumbu ya mahojiano
34. Hati ya dhamana ya shahidi
35. Upekuzi na afisa polisi
36. Uwezo wa kuchukuwa alama za vidole, picha n.k
37. Uchunguzi wa kitabibu
38. Gwaride la utambuzi
39. Mamlaka ya kukagua leseni na kupekuwa magari
40. Jeshi kuweka amri kwenye barabara za umma.
41. Vikwazo vya barabara
42. Mamlaka ya kudhibiti muziki na vitendo vya mikusanyiko n.k
43. Mikusanyiko na maandamano sehemu za hadhara
44. Mamlaka ya kutawanya mikusanyiko na maandamano popote
inapofanyika
45. Wakati mikusanyiko au maandamano ni kinyume na sheria
46. Adhabu
SEHEMU YA TANO
MALI ZISIZODAIWA
47. Kuachiwa kwa mali zisizodaiwa.
SEHEMU YA SITA
MASHTAKA DHIDI YA MAAFISA POLISI
48. Kutokuwajibika kisheria kwa kitendo kilichofanyika chini ya mamlaka ya hati.
49. Mshahara wa maafisa polisi fulani kutokuchukuliwa kwa ajili ya pesa zilizokopwa au bidhaa zilizopelekwa.
SEHEMU YA SABA
NIDHAMU
50. Makosa ya nidhamu
51. Mamlaka ya afisa kufanya uchunguzi
52. Taratibu za uchunguzi
53. Adhabu za makosa ya nidhamu
54. Mamlaka maalum ya Mrakibu Mkuu
3
55. Mamlaka ya afisa anayefanya uchunguzi
56. Rufaa ya adhabu ya makosa ya nidhamu
57. Kuzuia kukisubiri uchunguzi na kusimamishwa.
58. Afisa aliyezuiwa au kusimamishwa kuendelea kuwa afisa polisi.
59. Kufukuzwa au kushushwa cheo kwa maafisa polisi wanapotiwa hatiani.
60. Faini kupatikana kwa kuzuia malipo.
61. Hasara au uharibifu wa silaha na vifaa vya askari kulipwa kwa
kuzuia malipo.
62. Kutokuwepo na malipo wakati wa kukosa kazini bila livu, kifungo au
kuwekwa kizuizini
63. Sehemu ya kuwafunga wahalifu.
64. Namna ya malalamiko la afisa polisi
65. Katazo dhidi ya afisa polisi kuwa mwanachama wa chama cha
wafanyakazi.
SEHEMU YA NANE
MFUKO WA TUZO WA POLISI
66. Kuanzishwa kwa Mfuko wa Tuzo wa Polisi.
SEHEMU YA TISA
VIINUA MGONGO NA STAHILI AMBAZO ZINAWEZA KUTOLEWA KWA WANACHAMA FULANI WA JESHI AMBAO SIO MAAFISA WANAOSTAHILI MALIPO YA UZEENI.
67. Utumikaji wa vifungu vya 68 hadi 72.
68. Viinua mgongo vinavyolipwa baada ya miezi kumi na mbili au zaidi ya
utumishi.
69. Viinua mgongo vyenye uwiano vinavyolipwa katika mazingira fulani.
70. Viinua mgongo vilivyopatikana kuchukuliwa kuwa kama sehemu ya mali
ya afisa.
71. Viinua mgongo visivyolipwa mpaka kifo: mpangilio uko je.
72. Fidia panapotokea kifo, dhara au uharibifu unaotokea akiwa kazini.
73. Kiinua mgongo kwa waliopata tuzo.
SEHEMU YA KUMI
MPANGILIO/MGAWANYO WA MALI ZA MAREHEMU
74. Masharti ya mpangilio/mgawanyo wa mali ya maafisa waliokufa bila
wosia.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
AJIRA YA MAAFISA POLISI KWA KAZI MAALUMU NA KUDUMISHA AMANI SEHEMU ZENYE GHASIA
75. Ajira ya maafisa polisi kwa kazi maalumu kwa gharama za watu binafsi.
4
76. Ajira ya nyongeza ya polisi katika mazingira maalumu.
77. Ajira ya nyongeza ya polisi katika sehemu zenye ghasia.
78. Tuzo ya fidia kwa walioumia kutokana na vitendo vibaya vya wakazi wa
sehemu zenye ghasia.
79. Tafsiri ya"wakazi".
80. Upatikanaji na mgawanyo/ mpangilio wa pesa zilizolipwa chini ya
Sehemu ya XI.
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
AFISA POLISI MAALUMU
81. Mamlaka ya kuteua maafisa polisi maalumu.
82. Mamlaka ya kusimamisha kwa muda na kubainisha utumishi wa maafisa
polisi maalumu.
83. Raisi anaweza kuanzisha jeshi la maafisa polisi maalumu.
84. Tafsiri ya “afisa polisi maalumu".
85. Kukataliwa/kukataa kwa mtu aliyeteuliwa kutumika
86. Mamlaka na wajibu wa maafisa polisi maalumu.
87. Mrakibu Mkuu kuwapatia maafisa polisi maalumu vifaa muhimu.
88. Sare, n.k, kurudishwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha uteuzi.
89. Mrakibu Mkuu kusimamia/kutoa amri.
90. Kulipwa pale panapotokea kifo, dhara, uharibifu wa mali akiwa kazini.
SEHEMU YA KUMI NA TATU
UTUMISHI NJE YA JAMHURI YA MUUNGANO
91. Waziri anaweza kuwapeleka maafisa polisi nchi jirani.
92. Kupeleka maafisa polisi nchi jirani wakati wa dharura ya muda.
93. Maafisa polisi wanaotumikia nje ya Jamhuri ya Muungano kuwa chini ya
maafisa wao wenyewe na kwa kufuata sheria na amri zao wenyewe.
94. Masharti tangulizi kutimizwa na sheria ya nchi husika.
95. Maafisa polisi kutoka nchi jirani wanaotumikia Jamhuri ya
Muungano kuwa chini ya sheria zao, amri na maafisa wao wenyewe.
96. Utekelezaji wa mkataba uliofanywa na Serikali ya nchi jirani.
97. Mamlaka ya wanachama wa jeshi la polisi la nchi jirani.
98. Mamlaka ya mahakama za Jamhuri ya Muungano.
SEHEMU YA KUMI NA NNE
MASHARTI YA JUMLA
99. Mamlaka ya kuendesha mashtaka chini ya sheria nyingine kutodhurika.
100. Uasi.
101. Maafisa polisi walioondolewa kati ya tarehe fulani kutakiwa kuripoti.
102. Kutelekeza.
103. Kumiliki kusiko halali kwa vifaa walivyopewa afisa polisi na uhuishaji
kinyume na sheria.
104. Kuwaweka katika nyumba za umma maafisa polisi wakati wakiwa kazini
5
105. Watu wanaosababisha chuki, n.k.
106. Vitendo visivyokubalika katika kituo cha polisi, ofisini au mahabusu 107. Adhabu ya jumla.
SEHEMU YA KUMI NA TANO
AKIBA YA POLISI
108. Kuanzishwa kwa Akiba ya Jeshi.
109. Muundo wa Akiba
110. Udhibiti wa Akiba
111. Tangazo kutolewa wakati wa uandikishwaji
112. Kipindi cha utumishi katika Akiba
113. Cheo kugawiwa kwa askari wa akiba
114. Haki ya kujiondoa katika mazingira fulani
115. Malipo na posho
116. Wajibu wa askari wa akiba
117. Kuondoa Akiba ya polisi kwa mafunzo ya mwaka
118. Kuondoa Akiba ya polisi kwa ajili ya kutumika wakati wa
dharura.
119. Wanapoitwa kwa ajili ya mafunzo au utumishi, taarifa kutolewa
kwa akiba ya polisi.
120. Pale ambapo Akiba ya polisi wanaondolewa chini ya masharti ya Sheria
hii.
121. Adhabu.
122. Kuondolewa kwa Akiba ya polisi.
123. Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kuacha kutumia utumishi wa Akiba ya
polisi
124. Viinua mgongo.
SEHEMU YA KUMI NA SITA
JESHI LA POLISI SAIDIZI
125. Tafsiri
126. Kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi Saidizi.
127. Kazi za Jeshi la Polisi Saidizi.
128. Mamlaka ya Jumla ya Mrakibu Mkuu.
129. Kutangazwa kwa sehemu maalumu.
130. Jeshi la Polisi Saidizi kuwekwa katika maeneo maalumu.
131. Kuanzishwa na kudumishwa kwa vituo vya polisi katika maeneo maalum.
132. Maeneo maalum kuchukuliwa kuwa moja ya mazingira fulani.
133. Utawala na udhibiti wa jeshi la polisi saidizi katika maeneo maalum.
134. Kuteuliwa kwa maafisa wa jeshi la polisi saidizi.
135. Kujiuzulu.
136. Kufutwa kwa mwongozo
137. Malipo ya polisi saidizi.
138. Vifaa.
6
139. Mamlaka, Wajibu na kinga ya polisi saidizi.
140. Makosa ya nidhamu.
141. Mamlaka ya kukamata kwa utendaji makosa.
142. Adhabu zinazoweza kutolewa.
143. Kuwasilisha begi, mwongozo,na sare baada ya kujiuzulu, n.k.
144. Kurudishwa kwa begi, mwongozo na sare zilizowasilishwa
145. Makosa.
146. Afisa polisi kwa madhumuni ya kifungu cha 243 cha Sheria ya Kanuni za
Adhabu
147. Mamlaka ya Jeshi la Polisi chini ya Sehemu hii kuwa nyongeza.
SEHEMU YA KUMI NA SABA
MASHARTI YA KAWAIDA
148. Kanuni.
149. [Kufutwa kwa R.L. Sura ya 55 na 59.]
MAJEDWALI
7
SURA YA 322
SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI
Sheria ya kuweka utaratibu, nidhamu, mamlaka na wajibu wa Jeshi la Polisi, Polisi wa Akiba na Jeshi la Polisi lisaidialo na mambo yanayohusiana.
[Januari 1, 1953]
[Agosti 13, 1939]
[Juni 9, 1948]
Sheria . Namba.
1 ya 1939
14 ya 1950
51 ya 1952
27 ya 1954
22 ya 1955
1 ya1958
43 ya 1958
[R.L. SURA YA 56]
[R.L. SURA YA 262]
64 ya 1961
35 ya 1962
19 ya 1964
35 ya 1965
73 of 1965
Gazeti la serikali Na. 73 la 1965
[R.L. SURA YA 322]
Sheria Na .
2 ya 1965
19 ya 1965
11 ya 1971
31 ya 1972
15 ya 1980
9 ya 1985
5 ya 1993
3 ya1995
8
[SURA ya 322] SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI
_______________________________________________________________________
.
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA MWANZO
1. Jina fupi na utumikaji
(1) Sheria hii itaitwa Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi
(2) Vifungu vifuatavyo vitatumika Tanzania Bara na Visiwani
Vifungu vya 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 16, 26, 63, 64, 66 (3) na (4), 67, 68, 69, 70, 71, 72, 73, 74, 81, 82, 83, 84, 85, 86, 87, 88, 89, 90, 91, 92, 93, 94, 95, 96, 97, 98, 100 na 106.
2.Tafsiri Sheria Na. 22 ya 1955 kifungu cha 2; 1 ya 1958 kifungu cha 2; Gazeti la Serikali Na . 73 ya 1965; 11 ya 1971; 31 ya 1972; 73 ya 1965; 15 ya 1980; 9 ya 1985; 5 ya 1993
2. Katika Sheria hii, kama itahitaji vinginevyo:-
"silaha" ni pamoja na silaha ya moto;
"Kamishna Msaidizi" maana yake ni Kamishna Msaidizi wa Polisi na msemo huu ni pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Inspekta msaidizi au afisa polisi mwingine ambaye ni mkuu/kamanda wa kundi la askari katika mkoa wowote; na "Kamishna " maana yake ni Kamishna Mwandamizi au Kamishna aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 8;
"kosa tambuzi" ina maana iliyotajwa katika kifungu cha 2 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai *;
"polisi wa daraja la chini" ni pamoja na askari wote wenye hadhi ya daraja la chini ;
"Naibu Kamishna" maana yake ni Naibu Kamishna wa Polisi;
"Jeshi" maana yake Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano;
"Afisa aliyeandikwa kwenye Gazeti la Serikali" maana yake ni afisa polisi wa daraja la inspekta msaidizi au zaidi ;
"inspekta" ni pamoja na inspekta mkuu, inspekta mwandamizi, inspekta na inspekta msaidizi;
"Inspekta Jenerali" maana yake ni Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi;
"kileo " ina maana iliyotajwa katika Sheria ya Vileo*;
"Waziri " maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya mambo yanayohusiana na Jeshi la Polisi;
"afisa asiyekuwa na cheo" maana yake ni afisa polisi wa daraja la sajini meja, sajini au koplo;
"afisa msimamizi wa polisi" maana yake ni afisa polisi aliyeteuliwa na Kamishna chini ya kifungu cha 8 kuliongoza jeshi la polisi katika sehemu yoyote, au afisa polisi mwandamizi yeyote kwa wakati huo na mahali hapo; na pale ambapo hakuna afisa polisi aliyeteuliwa kama ilivyosemwa hapo juu, ni pamoja na afisa mtawala msimamizi wa mahali hapo kwa wakati huo;
9
"afisa msimamizi wa kituo cha polisi"ni pamoja na afisa yeyote wa daraja la juu ya afisa mkubwa kwa daraja la afisa msimamizi wa kituo cha polisi na, pale afisa msimamizi wa kituo hayupo katika kituo cha kazi au ameshindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na ugonjwa au sababu nyingine yoyote, afisa polisi atakayekuwepo katika kituo hicho anayemfuata kwa daraja ofisa polisi huyo;
"afisa anayestahili pensheni" maana yake ni mwanachama wa Jeshi ambaye utumishi wake unastahili pensheni chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma na Stahili za Kustaafu*;
"afisa polisi" maana yake ni mwanachama yeyote wa Jeshi wa daraja la konstebo/chini au zaidi;
"kituo cha polisi" maana yake ni sehemu yoyote iliyoteuliwa na Mrakibu wa polisi/Inspekta Generali Mkuu kuwa kituo cha polisi;
"Mfuko wa Polisi wa Tuzo" maana yake ni Mfuko ulioanzishwa chini ya kifungu cha 66 cha Sheria hii;
"stesheni/Kituo cha polisi" maana yake ni sehemu yoyote iliyoteuliwa na Inspekta Jenerali Mkuu kuwa stesheni,kituo cha polisi, na inajumuisha sehemu yoyote inayolindwa na stesheni/kituo hicho;
"iliyoelekezwa" maana yake iliyoelekezwa na kanuni zilizotengenezwa chini ya Sheria hii;
"mali" inajumuisha mali yoyote inayohamishika, pesa au amana ya thamani;
"mahali pa umma" maana yake ni barabara yoyote kuu, maegesho ya umma, bustani, ufukweni mwa bahari, pwani ya ziwa na daraja lolote la umma, barabara, mtaa, barabara nyembamba, njia ya miguu, mraba, kitala, kichochoro au njia ama ya kupita au la; pia inajumuisha sehemu yoyote iwe jengo au la, ambapo kwa wakati huo umma unaruhusiwa kuutumia ama kwa malipo au vinginevyo;
"kuruta" maana yake ni mtu anayechukuwa mafunzo kwa ajili ya kazi ya Jeshi na ambaye ni mwanachama wa Jeshi lakini ambaye sio afisa polisi;
"mkoa" maana yake mkoa katika Jamhuri ya Muungano ambapo usimamizi wa polisi uko chini ya Kamishna Msaidizi au Mrakibu au afisa polisi mwingine aliyeteuliwa na Inpekta Jenerali Mkuu kuwa msimamizi katika mkoa huo;
"sajini" ni pamoja na Sajini wa kituo na sajini wa madaraja yote ya cheo cha sajini;
"Mrakibu" ni pamoja na Inspekta Mwandamizi;
"Mrakibu Msimamizi wa Polisi" maana yake ni Inspekta au afisa polisi mwingine aliyeteuliwa na Inspekta Jenerali Mkuu kuwa msimamizi wa tawi lolote la Jeshi au stesheni zote za polisi katika mkoa.
10
SEHEMU YA PILI
MUUNDO, UTAWALA NA WAJIBU WA JESHI LA POLISI
Kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi Gzt la Ser..Na. 73 la 1965
3. Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litaanzishwa na kuundwa kulingana na na Sheria hii.
Muundo wa Jeshi Gzt.Na. 73 ya 1965 Jedwali la pili; Sheria Na. 11 ya 1971 Jedwali; Gzt.Na. 19 ya 1966; 19 ya 1996
4. Jeshi litaundwa na wanachama wa madaraja yafuatayo kama Rais atakavyoelekeza, katika mpangilio ufuatao wa uandamizi-
Maafisa waliochapishwa katika Gazeti la Serikali:-
Inspekta Jenerali Mkuu
Kamishna
Kaimu Kamishna
Kamishna Msaidizi
Inspekta Mwandamizi
Inspekta
Inspekta Msaidizi
Mainspekta:-
Inspekta Jenerali Mkuu
Inspekta Wasaidizi
Maafisa Wasiokuwa na Vyeo:–
Sajini Meja
Afisa Sajini
Sajini
Koplo
Polisi daraja la chini:-
Askari Polisi wa daraja la chini
Kuruta
Mwanafunzi katika shule ya maofisa wa Jeshi la Polisi
Wajibu wa Jeshi la Police Gzt. Na. 73 ya 1965 Jedwali la 2.
5.-(1) Jeshi la Polisi litaajiriwa ndani na katika Jamhuri yote ya Muungano kwa ajili ya kulinda amani, kudumisha sheria na utulivu, kuzuia na kugundua uhalifu, kuwakamata na kuwaongoza watuhumiwa na kulinda mali, na katika utekelezaji wa majukumu yote hayo watakuwa na haki ya kubeba silaha.
(2) Wanachama wote wa Jeshi watalazimika kutumikia popote pale katika Jamhuri ya Muungano a au kwenye meli ndani ya mipaka ya maji ya Jamhuri ya Muungano , na kuendelea katika nchi yoyote ya jirani kama ilivyoelezwa katika Sehemu ya XIII ya Sheria hii, na kuendelea katika sehemu nyingine kama majukumu yao chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki kama kitakavyohitaji
Imefutwa
6. Imefutwa na Sheria Na. 2 ya 1965 Jedwali la 2.]
Mamlaka ya jumla ya Inspekta
7.- (1) Inspekta Jenerali Mkuu atakuwa kutegemea maagizo au maelekezo ya Waziri kama msimamizi wa kiutendaji wa Jeshi na atatoa amri, usimamizi na
11
Jenerali Mkuu Gzt. Na. 148 ya 1961; 73 ya 1965 Jedwali la 2.
maelekezo kwa Jeshi.
(2) Inspekta Jenerali Mkuu anaweza , kwa kutegemea maagizo au maelekezo ya Waziri na katika masharti ya sheria hii na kanuni zozote zilizotengenezwa, mara kwa mara ataweka maagizo kwa serikali yote ya Jeshi kulingana na uandikishwaji, madaraja, majukumu, usambazaji, upekuzi, uhamisho, ( ikijumuisha gharama zote zinazohusiana) kuondoa, mafunzo, silaha na vifaa vyote vya askari, mavazi na vifaa, na sehemu za makazi ya wanachama wa Jeshi, na maagizo mengine anayoona yanafaa kwa ajili ya kuzuia uzembe na kuimarisha ufanisi na nidhamu sehemu ya Jeshi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Utawala wa Jeshi Gzt. Na. 73 ya 1965 Jedwali la pili; Sheria Na. 11 ya 1971.
8.-(1) Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakuwa chini ya utawala wa Mrakibu Mkuu, na kwa dhumuni hili, Jeshi litaandaliwa katika matawi yote na kusambazwa kutokana na mahitaji ya Mkoa husika, na sehemu nyingine kama atakavyoamua, kwa idhini ya Waziri.
(2) Kamishna anaweza kuteuliwa kwa ajili ya sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano, au kwa ajili ya kazi yoyote ya Jeshi, na Kamishna atakayechaguliwa atakuwa Kaimu wa Inspekta Jenerali Mkuu, na kwa sehemu hiyo , au kwa madhumuni ya kazi hiyo, kama itakavyoweza kuwa, kwa kuzingatia maelekezo yoyote ya Inspekta Jenerali Mkuu, atakuwa na mamlaka, kazi, na wajibu wa Inspekta Jenerali Mkuu badala yake; na pale ambapo Kamishna ameteuliwa kwa ajili ya sehemu yoyote ile, makamanda wasaidizi watawajibika kwa Inspekta Jenerali Mkuu na Kamishna kwa heshima zao stahili na masharti yafuatayo katika kifungu hiki yatatafsiriwa kama yalivyo. [kifungu.(1A)]
(3) Pale ambapo Kamishna Mwandamizi ameteuliwa kwa ajili ya sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano au kwa ajili ya kazi yoyote ya Jeshi, masharti ya kifungu kidogo cha (2) yatatumika kulingana na Kamishna Mwandamizi kana kwamba marejeo katika kifungu hicho kidogo kwa Kamishna huyo yalikuwa ni marejeo kwa Kamishna Mwandamizi, na kila Kamishna aliyeteuliwa kwa ajili ya sehemu hiyo ya Jamhuri ya Muungano au kwa ajili ya kazi hiyo atawajibika kwa Kamishna Mwandamizi.
[Kifungu cha (1B)]
(4) Kamanda wa Polisi katika Mkoa wowote atakuwa na mamlaka kama ya Kamishna Msaidizi au Inspekta msimamizi au afisa polisi yeyote aliyeteuliwa na Kamishna kuwa kamanda katika eneo husika. Kwa kuzingatia amri na maelekezo ya Kamishna na, itakapotokea afisa polisi kamanda wa Mkoa , au Kamishna Msaidizi, au afisa polisi msimamizi yeyote wa mkoa, ambaye yuko katika eneo hilo, afisa polisi huyo atakuwa na usimamizi, maelekezo na uongozi wa polisi katika mkoa alioteuliwa, na atawajibika kwa Inspekta Jenerali Mkuu na, pale ambapo afisa polisi msimamizi katika mkoa, na kwa afisa polisi msimamizi wa mkoa ambaye atakuwa katika eneo hilo, kwa mambo yote yanayohusiana na mafunzo, nidhamu na uchumi wa ndani wa wanachama na Jeshi chini ya usimamizi wake, utendaji na wajibu wa polisi katika mkoa wake au eneo lake kama itakavyokuwa.
[kifungu cha (2)]
12
(5) Utawala/usimamizi wa polisi katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakabithiwa afisa polisi kama atakavyoteuliwa na Kamishna kuwa msimamizi katika eneo hilo. Afisa polisi huyo atakuwa msaidizi na kutekeleza amri za afisa polisi kamanda katika jimbo ambalo liko katika sehemu hiyo, katika mambo yote yanayohusiana na mafunzo, nidhamu na uchumi wa ndani wa wanachama wa Jeshi chini ya usimamizi wake, na utendaji wa wajibu wote wa polisi katika mkoa wake au eneo lake katika sehemu iliyotajwa. [kifungu cha (3)]
(6) Katika sehemu yoyote ambayo hakuna afisa polisi aliyeteuliwa na Inspekta Jenerali Mkuu kuwa kamanda wa polisi katika sehemu hiyo, afisa tawala msimamizi wa wakati huo katika eneo hilo atakuwa na mamlaka hayo kisheria zaidi ya afisa msimamizi wa polisi kama itakavyokuwa lazima kwa madhumuni ya utekelezaji, na, kwa kuzingatia amri na maelekezo ya afisa polisi mtawala katika mkoa ambapo sehemu hiyo ipo, atakuwa na utawala katika jeshi hilo la polisi ikiwa ni pamoja na mafunzo yao, nidhamu, na uchumi wa ndani:
Isipokuwa kwamba hakuna chochote katika sehemu ya I hadi ya XIV ya Sheria hii kitakachoweza kumzuia afisa tawala au afisa polisi.
[kifungu cha (4)]
(7) Pale ambapo afisa tawala amekaimishwa mamlaka na wajibu wa afisa msimamizi atatunza vitabu na kupeleka mahesabu kama Mrakibu Mkuu atakavyoelekeza mara kwa mara. [kifungu cha (5)]
Uwakilishi wa Inspekta Jenerali Mkuu Gzt. Na. 73 ya 1965 Jedwali la Pili.
9. Kamishna anaweza, kwa makubaliano na Waziri, na kwa maandishi yake mwenyewe, kunaibisha mamlaka yake yoyote yaliyopo katika sehemu ya I hadi ya XIV ya sheria hii ili kwamba mamlaka yaliyonaibishwa yanaweza kutekelezwa na aliyenaibishwa katika mambo au kundi la mambo yaliyoainishwa au kutafsiriwa katika chombo cha unaibishaji.
Maafisa wasimamizi wa kituo cha polisi kutunza vitabu husika na kutoa ripoti Gzt. Na. 73 ya 1965
10. Afisa msimamizi yeyote wa kituo cha polisi atatunza kitabu cha jumla cha kumbukumbu au kitabu cha matukio, katika jinsi ambavyo Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kuelekeza mara kwa mara, na ataweka katika kumbukumbu malalamiko na mashtaka yote yaliyoletwa, majina ya watu wote waliokamatwa na makosa waliyoshtakiwa nayo, pia atatunza vitabu hivyo na kumbukumbu na atatoa ripoti hiyo kwa Inspekta Jenerali Mkuu kama atakavyoweza kuelekeza mara kwa mara.
Maafisa polisi wasimamizi kuwajibika na vifaa/zana Gzt. Na. 73 ya 1965
11. Afisa polisi yeyote msimamizi atawajibika na vifaa na pesa zote za umma zilizotolewa na kupelekwa kwa matumizi ya wanachama wa jeshi chini ya usimamizi wake na atatoa hesabu ya vitu hivyo kwa Inspekta Jenerali Mkuu
SEHEMU YA III
UTEUZI, UANDIKISHWAJI, UTUMISHI NA KUONDOLEWA
(kifungu cha 12-26)
Uteuzi wa Maafisa polisi
12. (1) Maafisa waliochapishwa katika gazeti la Serikali watateuliwa na Jeshi la Polisi na Tume ya Utumishi wa Magereza iliyoanzishwa chini ya sheria ya
13
Jeshi la Polisi na Tume ya Utumishi wa Magereza*.
(2) Mainspekta na maofisa polisi wasiokuwa na cheo watateuliwa na Inspekta Jenerali Mkuu kwa jinsi ambavyo Waziri anaweza kuelekeza na kwa kuzingatia masharti hayo (kama yatakuwepo) kama yanavyoweza kuainishwa katika sheria hii na kanuni na amri zozote zilizowekwa chini ya sheria hii.
Muda wa utumishi wa mrakibu Sheria Na, 1 ya 1958 kifungu cha 4
13. Kila inspekta baada ya kuteuliwa atatumikia Jeshi kwa muda wa majaribio usiopungua miaka miwili mfululizo katika huduma na muda mwingine utakaoongezwa kama itakavyoweza kupangwa na Inspekta Jenerali Mkuu.
Uandikishwaji wa askari polisi, wafualitiliaji na wanafunzi katika Jeshi la Polisi Sheria Na. 22 ya 1955 kifungu cha. 4
14. (1) Kila askari polisi na mfuatiliaji ataandikishwa kutumikia Jeshi kwa kipindi cha miaka mitatu, au kipindi kingine chochote kifupi zaidi kama itakavyoweza kupangwa na Waziri.
(2) Kila mwanafunzi katika jeshi la polisi ataandikishwa kutumikia Jeshi kipindi cha miaka saba, au kipindi kingine chochote kifupi zaidi kama itakavyoweza kupangwa na Waziri.
(3) Hakuna mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane anaweza kuandikishwa katika Jeshi bila ya kupata kwanza kibali kutoka kwa mzazi au mlezi wake au, kama mzazi au mlezi wake hawezi kupatikana, itolewe idhini kwanza na Mkuu wa Wilaya katika wilaya ambayo mtu huyo anaishi
Azimio katika kujiunga na Polisi
15. (1) Ofisa polisi yeyote aliyeteuliwa au aliyeandikishwa chini ya masharti ya Sehemu hii, wakati wa kujiunga na Jeshi, atatengeneza na kusaini azimio mbele ya hakimu au afisa aliyeandikishwa katika gazeti la serikali katika jinsi ambavyo anaweza kutoa ahadi kamili akiwa na akili timamu katika fomu Na. 1 ya Jedwali la Kwanza la Sheria hii.
(2) Afisa polisi yeyote baada ya kuteuliwa au kuandikishwa kama ilivyosemwa hapo juu na kabla ya kuweka azimio linalohitajika na kifungu kidogo cha (1), atatakiwa kujibu ukweli maswali yote anayoweza kuulizwa kuhusu utumishi wake wa nyuma katika Jeshi na pengine kama alishawahi kupatikana na hatia katik kosa lolote la jinai.
(3) Mtu yeyote ambaye kwa kudhamiria atasema uongo katika kujibu swali aliloulizwa chini ya kifungu kidogo cha (2) atakuwa na hatia na atahukumiwa kutoa faini isiyozidi shillingi mia mbili au kifungo cha mwezi mmoja.
Masharti ya likizo Gzt. Na. 73 ya 1965
16. Wanachama wa Jeshi wa daraja la chini ya mrakibu atastahili kupata likizo kulingana na kanuni zitakazokuwepo chini ya sheria hii.
Kuajiriwa upya
17. (1) Mwanachama yeyote wa Jeshi mwenye tabia nzuri, tofauti na afisa anayestahili malipo ya uzeeni, ambaye amemaliza kipindi chake kilichoandikishwa, anaweza, kwa idhini ya Inspekta Jenerali Mkuu, kuajiriwa upya kwa kipindi kingine kisichozidi miaka mitatu, na anaweza pia kuajiriwa tena kwa mara ya tatu au kipindi chochote kitakachofuata mpaka atakapomaliza miaka kumi na mbili ya utumishi.
(2) Mwanachama yeyote ambaye atakuwa ametajwa katika kifungu
14
kidogo cha (1) anaweza, kwa idhini ya Mrakibu Mkuu, baada ya kumaliza kipindi hicho cha miaka kumi na mbili kuajiriwa tena kwa vipindi vingine kama itakavyoweza kupangwa na Inspekta Jenerali Mkuu mpaka pale atakapomaliza kipindi kinachojumuisha miaka ishini na moja ya utumishi.
(3) Mwanachama yeyote ambaye atakuwa ametajwa katika kifungu kidogo cha (2) anaweza, kwa idhini ya Inspekta Jenerali Mkuu, baada ya kumaliza miaka ishini na moja, kuendelea kuwepo katika Jeshi kwa namna hiyohiyo na kwa heshima zote kama vile muda wake wa utumishi haujamalizika, isipokuwa kwamba itakuwa halali kwake yeye, kufuatia masharti yaliyopo katika kifungu cha 22, kudai kuondolewa kwake baada ya kumalizika kwa miezi mitatu na baada ya kutoa taarifa, kwa afisa msimamizi wa polisi katika kituo chake cha kazi, kuhusu matakwa ya kuondolewa kwake.
Kuajiriwa upya baada ya kuondolewa
18. (1) Mwanachama yeyote wa Jeshi zaidi ya afisa anayestahili malipo ya uzeeni anaweza, kwa idhini ya Inspekta Jenerali Mkuu, kuajiriwa upya kwa utumishi katika kipindi cha miezi sita baada ya kupata taarifa ya kuondolewa kwake na, kama Inspekta Jenerali Mkuu ataidhinisha kuajiriwa kwake upya, atakuwa na haki, kufuatia kuweko kwa nafasi hiyo, ya daraja au cheo alichokuwa nacho tarehe ya kuondolewa kwake; na utumushi wake utachukuliwa kuwa endelezi kwa madhumuni ya malipo ya uzeeni au kiinua mgongo.
(2) Kama kutakuwa na mwanachama wa Jeshi ambaye atakuwa ameruhusiwa kuajiriwa upya baada ya kumalizika kwa miezi sita kuanzia tarehe ya kuondolewa kwake, Inspekta Jenerali Mkuu, anaweza, kufuatia idhini ya Waziri, kuruhusu utumishi wake wa nyuma au sehemu ya utumishi huo kuhesabika kwa madhumuni ya malipo ya uzeeni au kiinua mgongo, na swala la kumrudisha kwenye daraja au cheo alichokuwa nacho katika tarehe aliyoondolewa ataachiwa Inspekta Jenerali Mkuu.
Utumishi katika jeshi lingine la polisi yaweza kuhesabika kama utumishi katika Jeshi.
19. Kama mwanachama yeyote wa Jeshi tofauti na afisa anayestahili pensheni ambaye siku za nyuma ametumikia kama afisa polisi katika muundo wa utumishi wa polisi ulio sawa na Koloni lolote la Kiingereza au nchi iliyo chini ya utawala wa nchi nyingine au taifa linalolindwa, au nchi yoyote iliyo chini ya utawala wa kiingereza, ameandikishwa katika Jeshi miezi sita baada ya kuondolewa katika utumishi huo wa nyuma, kufuatia idhini ya Waziri , ataruhusiwa kuhesabu kipindi chake cha utumishi cha nyuma katika koloni husika, nchi iliyochini ya utawala wa nchi nyingine, taifa au nchi, kama vile ulikuwa utumishi wa Jeshi:
Isipokuwa kwamba hakuna mwanachama wa Jeshi atakayeruhusiwa kuhesabu kiinua mgongo katika kipindi cha utumishi pale ambapo kiinua mgongo kimeshalipwa au pensheni imekuwa ikilipwa kutoka kwenye mfuko wa koloni, nchi iliyo chini ya utawala wa nchi nyingine au taifa
Maafisa Polisi kutokujiuzulu bila ruhusa
20. Hakuna mwanchama wa Jeshi mwenye daraja la chini ya msimamizi msaidizi atakuwa na uhuru wa kujiuzulu kutoka katika Jeshi wakati anatumikia kipindi chake cha kuajiriwa au kuajiriwa upya isipokuwa kama imeruhusiwa kufanya hivyo na Inspekta Jenerali Mkuu, au afisa mwingine
15
ambaye ana mamlaka ya kutoa ruhusa hiyo.
Wanachama wa Jeshi kutokujihusisha na ajira nyingine.
21. Hakuna mwanachama wa Jeshi, bila ya kibali cha Inspekta Jenerali Mkuu, atajihusisha na ajira nyingine yoyote ile au ofisi kwa namna yoyote isipokuwa kwa kufuatia wajibu wake chini ya Sheria hii.
Kurefushwa kwa utumishi inapotokea vita.
22. Bila kujali kifungu kingine chochote cha sehemu ya I - XIV ya sheria hii, afisa polisi yeyote ambaye kipindi chake cha utumishi kimemalizika wakati wa vita, maasi au uadui anaweza kubaki na utumishi wake unaweza kurefushwa kwa kipindi hicho cha ziada, kinachomalizika katika muda usiozidi miezi sita baada ya kukoma kwa vita, maasi au uadui, kama Waziri atakavyoelekeza.
Kuondolewa Sheria. Na. 1 ya 1958 kifungu cha 5
23. (1) Kufuatia masharti ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu hiki, mwanachama yeyoye wa Jeshi tofauti na afisa aliyeandikishwa kwenye gazeti la serikali anaweza kuondolewa na Inspekta Jenerali Mkuu muda wowote:–
(a) kama Inspekta Jenerali Mkuu amefikiria kuwa hawezi kuwa mtendaji bora au ameacha kuwa afisa polisi mtendaji bora;
(b) kama amedhibitishwa na afisa tabibu wa Serikali kuwa hayuko sawa kiakili na kimwili kwa ajili ya kuhudumua zaidi katika Jeshi;
(c) katika kulipa kuondolewa kwake, kwa idhini ya Inspekta Jenerali Mkuu , katika viwango vilivyoorodheshwa katika Jedwali la Pili la Sheria hii:
Isipokuwa kwamba iwapo katika tarehe ya kulipa kuondolewa kwa afisa huyo au mfuatiliaji hajamaliza kipindi chake cha utumishi alichoandikishwa kwa mara ya kwanza atarejesha fedha yote au sehemu ya gharama (kama itakuwepo) kama Inspekta Jenerali Mkuu atakavyobainisha gharama zilizogharamiwa na serikali kumleta katika Jamhuri ya Muungano:
Isipokuwa tena kwamba Inspekta Jenerali Mkuu atakuwa na mamlaka ya kusamehe malipo yote au sehemu ya malipo ya kuondolewa katika mazingira hayo na masharti hayo kama atakavyoona inafaa;
(d) Katika kupunguza kwa kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi.
(2) Hakuna mwanachama wa Jeshi la Polisi wa daraja sawa au zaidi ya Mrakibu Mdogo ataondolewa chini ya kifungu hiki bila idhini ya Waziri.
(3) Waziri anaweza, katika wakati wowote kwa amri, kurekebisha Jedwali la Pili katika Sheria hii.
Masharti katika kuhesabu makosa ya utumishi kwa ajili ya kuondolewa.
24. Katika kuhesabu makosa ya utumishi ya mwanachama yeyote wa Jeshi zaidi ya afisa anayestahili malipo ya uzeeni kwa ajili ya kuondolewa vitatolewa vipindi vyote ambavyo mwanachama huyo wa Jeshi ambavyo hakuwepo kazini kutokana na sababu zifuatazo:-
(a) Kifungo kwa sababu yoyote ukiachilia kifungo kwa sababu yoyote isipokuwa kifungo cha kusubiri mashtaka yoyote ambayo yamepelekea kuchiliwa huru au kuondolewa;
16
(b) Kutelekeza;
(c) Kukosa kazini bila likizo kwa muda unaozidi saa arobaini na nane.
Kuondolewa baada ya kipindi cha utumishi kumalizika.
25. (1) Kufuatana na masharti yaliyopo katika vifungu vya 17, 18, 19 na 22, kila mwanachama wa Jeshi, tofauti na afisa anayestahili malipo ya uzeeni, ambaye amemaliza kipindi au vipindi vya utumishi kulingana na masharti ya Sehemu ya I hadi yaXIV ya Sheria hii, ataondolewa na afisa msimamizi wa kituo katika kituo alichopangiwa, isipokuwa kama siku ya tarehe ya kumalizika kwa utumishi huo anatumikia adhabu aliyohukumiwa kwa kutenda kosa lolote kinyume na nidhamu chini ya kifungu cha 50, ambapo kipindi chake cha utumishi kitarefushwa na kuondolewa kwake kutasimamishwa mpaka adhabu hiyo ifutwe au mpaka awe amemaliza mashtaka na ameachiwa huru au amepata adhabu yoyote ambayo inaweza kutolewa kulingana na kosa aliloshtakiwa.
(2) Kila mwanachama huyo wa Jeshi, wakati wa kuondolewa, atapewa cheti cha kuondolewa katika fomu iliyoagizwa na, mpaka atakapopata cheti hicho cha kuondolewa, atabaki kufuatana na masharti yaliyopo katika sheria hii.
Silaha na vifaa vyote vya askari kuwasilishwa vitakapokoma kuwa mali ya Jeshi. Sheria Na. 64 ya 1961 kifungu cha 4; Gzt. Na. 73 ya 1965 Jedwali la Pili.
26. (1) Pale mwanachama wa Jeshi atakapokoma kuwa mwanachama wa Jeshi, mamlaka yote na uwezo wa kisheria aliopewa wa kutenda jambo utakoma haraka na papohapo atawasilisha kwa mtu aliyeteuliwa na Inspekta Jenerali Mkuu kwa kusudi hilo au kwa afisa msimamizi wa polisi katika kituo ambacho ni cha mwisho kupangiwa silaha zote, risasi, vifaa vyote vya askari isipokuwa mavazi na silaha, mavazi, sare na samani nyingine atakazokuwa amepewa au kukabidhiwa kwa uangalifu wake na ambazo ni mali ya Serikali
(2) Mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye, baada ya kukoma kuwa mwanachama wa Jeshi, ameshindwa kuwasilisha silaha yoyote, risasi, vifaa vyote vya askari isipokuwa mavazi na silaha , mavazi, sare au samani nyingine kama inavyohitajika na kifungu hiki atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kwa kutoa fidia isiyozidi shilingi mia nne au kifungo cha miezi mitatu au kwa vyote fidia hiyo na kifungo hicho , na mahakama inaweza kutoa hati ya kupekuwa na kukamata silaha zote , risasi , vifaa vyote vya askari isipokuwa mavazi na silaha , mavazi, sare na samani nyingine ambazo zitakuwa hazijawasilishwa.
SEHEMU YA NNE
MAMLAKA NA WAJIBU WA MAAFISA POLISI
(Kifungu cha 27- 46)
Mamlaka ya jumla na wajibu wa maafisa polisi Gzt. Na. 73 ya 1965
27. (1) Kila afisa polisi atatekeleza mamlaka hayo na kutekeleza wajibu kama kisheria alivyotunukiwa au kupewa afisa polisi, na atatii maelekezo yote halali yanayohusiana na utekelezaji wake wa ofisi ambayo anaweza mara kwa mara kuyapata kutoka kwa wakubwa wake katika Jeshi.
17
Jedwali la Pili.
(2) Kila afisa polisi atahesabika kuwa kazini muda wote na anaweza katika muda wowote kufahamika kuwa kazini katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Kila afisa polisi atatii mara na kutekeleza amri zote na hati zote zilizotolewa kwake kihalali, atakusanya na kuwasiliana na maafisa wapelelezi wa daraja la juu wanaoathiri amani, atachukua hatua zote za muhimu kuzuia kutendeka kwa makosa na vurugu kwa umma na kupeleleza na kuwaleta wahalifu mahakamani wahukumiwe, na kuwakamata watu wote ambao ameruhusiwa kisheria kuwakamata na ambao ukamataji wake una sababu ya kutosha; na kwa makusudi yoyote yaliyotajwa katika kifungu hiki kidogo, bila ya hati, anaweza kuingia saa yoyote ya mchana au usiku katika jengo lolote lenye leseni chini ya Sheria ya Vilevi au sehemu yoyote ambapo ana sababu za msingi kutuhumu kwamba unywaji haramu au uchezaji wa kamari unafanyika mahali hapo au ulevi au tabia zisizokubalika zinatumika mahali hapo.
Afisa polisi kuchukuliwa kuwa afisa magereza katika mazingira fulani
28. (1) Pale ambapo afisa polisi anatekeleza majukumu ya afisa magereza, afisa polisi huyo, wakati akiwa katika jukumu hilo, atachukuliwa kuwa afisa magereza na atakuwa na mamlaka, ulinzi na marupurupu anayostahili afisa magereza huyo.
Maafisa polisi wanaweza kutumia silaha katika mazingira fulani
29. (1) Afisa polisi yeyote anaweza kutumia silaha dhidi ya:–
(a) mtu yeyote aliyefungwa kisheria kwa kutuhumiwa au kuhukumiwa kwa kosa pale ambapo mtu huyo anatoroka au anajaribu kutoroka na pale ambapo afisa polisi huyo ana sababu ya kutosha kuamini kwamba hataweza vinginevyo kuzuia utoro huo na amempa onyo mtu huyo kwamba angetumia silaha hizo dhidi yake na onyo hilo halikusikilizwa;
(b) mtu yeyote ambaye:–
(i) kwa kutumia nguvu, anaokoa au anajaribu kumuokoa mtu mwingine yoyote kutoka katika kifungo; au
(ii) kwa kutumia nguvu, anazuia au kujaribu kuzuia kukamatwa kwa mtu mwingine yeyote,
pale ambapo afisa polisi huyo ana sababu ya kutosha kuamini kwamba yeye au mtu mwingine yeyote yuko katika hatari ya kuumizwa na hataweza vinginevyo kukamata au kuzuia uokoaji huo
(2) Mamlaka aliyopewa afisa polisi chini ya kifungu hiki yatakuwa ni nyongeza na sio pungufu ya mamlaka yoyote aliyopewa afisa polisi huyo na sheria nyingine yoyote
Uwezo wa kutoa habari na malalamiko
30. Afisa polisi anaweza kutoa malalamiko halali au taarifa mbele ya hakimu na kuomba kuitwa shaurini, kibali, kibali cha upekuzi au hatua nyingine zozote za kisheria kama zitakazoweza kutolewa kisheria dhidi ya mtu yeyote
18
Sheria ya Dhamana ya Polisi Na.15 ya 1980.
31. (1) Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote inayotumika inayohusiana na kutolewa kwa dhamana na maafisa polisi, mtu aliyeletwa chini ya ulinzi wa polisi kwa tuhuma za kutosha kwamba ametenda kosa ataachiwa mara moja, pale ambapo:-
(a) afisa polisi aliyemkamata anaamini kwamba mtu huyo hakutenda kosa, au afisa polisi huyo hana sababu za kutosha za kuendelea kumuweka mtu huyo chini ya ulinzi;
(b) afisa polisi aliyemkamata anaamini kwamba alimkamata mtu ambaye siye;
(c) baada ya saa ishirini na nne baada ya mtu kukamatwa, hakuna mashtaka yaliyoletwa dhini ya mtu huyo, isipokuwa afisa polisi huyo anaamini kwamba kosa lililotuhumiwa kutendeka ni kubwa.
(2) Pale mashtaka yamesomwa dhidi ya mtu yeyote aliye chini ya ulinzi wa polisi, afisa polisi msimamizi wa kituo cha polisi anaweza, baada ya mtu huyo kupata dhamana, na wadhamini au bila wadhamini, kuwepo mahakama kama inahitajika, kumwondoa mtu huyo, pale ambapo:–
(a) mtu, japo alitakiwa kushtakiwa, alikamatwa bila hati maalum;
(b) baada ya upelelezi kukamilika, ushahidi usiokamilika, kuweka wazi shtaka lipi litaendelea;
(c) kosa ni kubwa ingawa si la hatari; au
(d) inaonekana kwamba upelelezi wa ziada lazima ufanyike, na hawataweza kumaliza ndani ya muda mfupi.
(3) Pale ambapo mtu aliyekamatwa ni wa umri chini ya miaka kumi na tano, mtu huyo anaweza kuachiwa baada ya mzazi, mlezi, ndugu au mtu yeyote wa kueleweka ameingia katika dhamana badala yake.
(4) Bila kujali sheria nyingine yoyote ambayo inatumika kuhusiana na kuidhinisha dhamana na maafisa polisi, hakuna ada au malipo yatatozwa kutokana na hati ya dhamana katika kesi za jinai, kupeleleza au kutoa ushahidi, au muonekano binafsi au ilivyotolewa vinginevyo kutolewa au kuchukuliwa na afisa polisi.
(5) Kila afisa polisi anayemkamata mtu anayetuhumiwa kutenda kosa lolote atamweleza mtu huyo haki yake ya dhamana chini ya kifungu hiki, na pale ambapo afisa polisi yeyote anakataa kuidhinisha dhamana kwa mtu yeyote aliye chini ya ulinzi, ataweka katika maandishi sababu zake za kukataa.
Mahudhurio ya mashahidi Sheria Na. 9 ya 1985 kifungu cha 397
32. (1) Pale ambapo afisa polisi anatuhumu kwamba mtu anaweza kuwa ametenda kosa kubwa, au anaamini kwamba habari imepokelewa na polisi ambayo inaweza kuhusisha mtu katika kutendeka kwa kosa kubwa, lakini tuhuma hizo au imani sio kama ilivyokuwa chini ya kifungu cha 13 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kudhibitisha uhalali wa kumkamata mtu bila hati, afisa polisi hatamuuliza maswali, isipokuwa amemfahamisha kwanza kwamba anaweza kukataa kujibu swali lolote analoulizwa na afisa polisi.
19
(2) Afisa polisi ambaye amemfahamisha mtu kama ilivyoelezwa chini ya kifungu kidogo cha (1) atamtaka mtu huyo kusaini au kutia dole gumba kama kukubali, kulingana na fomu zilizoidhinishwa, juu ya ukweli kwamba amefahamishwa na tarehe na wakati ambao alifahamishwa.
(3) Pale ambapo ni lazima kwa mahakama katika mashtaka yoyote, kuhakikisha endapo afisa polisi alimfahamisha mtu kama inavyohitajika na kifungu kidogo cha (1), na kukubali ilivyotajwa katika kifungu kidogo cha (2) na kusainiwa na mtu haijatolewa katika ushaidi, mahakama itachukulia, isipokuwa itadhibitishwa vinginevyo, kwamba mtu huyo hakufahamishwa.
(4) Bila kujali masharti ya kifungu hiki, pale ambapo afisa polisi katika harakati za kumhoji mtu yeyote kwa mujibu wa kifungu hiki anaamini kwamba kuna ushahidi wa kutosha kumkamata mtu huyo aliyeshtakiwa kwa kosa, ataendelea kumshtaki kwa kadiri ya sheria, na kumtahadharisha kwa maandishi au, kama inaweza kufanyika, kwa mdomo katika namna iliyowekwa na kumfahamisha kwamba ubaya unaweza kuchukuliwa kutokana na kushindwa kwake au kukataa kujibu swali lolote au kutokana na kushindwa kwake au kukataa kueleza katika hatua yoyote jambo lolote ambalo linaweza kuwa la msingi katika shtaka.
Kumbukumbu ya mahojiano Sheria Na. 9 ya 1985 kifungu cha 397
33. (1) Afisa polisi ambaye anamhoji mtu kwa dhumuni la kubainisha kama mtu ametenda kosa, isipokuwa katika mazingira yote haiwezekani kufanyika, atasababisha mahojiano hayo yakimalizika kuwekwa katika maandishi..
(2) Pale mtu ambaye amehojiwa na afisa polisi kwa dhumuni la kubaini endapo ametenda kosa, wakati wa mahojiano, iwe kwa mdomo au kwa maandishi, amekiri kufanya kosa, afisa polisi atafanya, au atasababisha kufanyika , wakati mahojianao yanaendelea, au mara baada ya mahojiano kukamilika, kuweka taarifa katika maandishi, ikionyesha:–
(a) ilimradi inawezekana kufanya hivyo, maswali aliyoulizwa mtu huyo wakati wa mahojiano na majibu yaliyotolewa na mtu kwa maswali hayo;
(b) ukamilifu wa maelezo yoyote yaliyotolewa na mtu kwa mdomo wakati wa mahojiano vinginevyo tofauti na jibu la swali;
(c) labda mtu aliandika maelezo yoyote wakati wa mahojiano na, kama hivyo, wakati ambao alianza kuandika maelezo hayo;
(d) labda onyo lilitolewa kwa mtu kabla ya kukiri kosa na, kama hivyo, masharti ambayo onyo lilitolewa, muda lililotolewa na majibu yaliyotolewa na mtu kwenye onyo;
(e) muda ambao mahojiano yalianza na kumalizika;
(f) kama mahojiano yalivurugwa, muda ambao yaliingiliwa na kuanza tena.
(3) Afisa polisi aliyechukuwa kumbukumbu ya taarifa ya mahojiano na mtu kulingana na kifungu kidogo cha (2) ataandika, au atahakikisha inaandikwa, mwisho wa mahojiano fomu ya cheti kulingana na fomu zilizoidhinishwa, na baadaye, isipokuwa kama mtu huyo hajui kusoma:–
(a) atamuonyesha kumbukumbu mtu huyo na kumtaka:–
(i) kuisoma na kufanya mabadiliko au masahihisho yoyote anayotaka kufanya na kuongeza maelezo yoyote ya ziada anayotaka kufanya;
20
(ii) kusaini cheti kilichotolewa mwisho wa taarifa; na
(iii) kama taarifa hiyo imezidi ukurasa mmoja, kuendelea na ukurasa mwingine ambao haujasainiwa na mtu huyo; na
(b) kama mtu anakataa, anashindwa au kuonekana kushindwa kukubaliana na ombi hilo, atathibitisha kwenye taarifa hiyo alichofanya na kuhusiana na mambo ambayo mtu huyo amekataa, ameshindwa au ameonekana kushindwa kukubaliana na ombi hilo.
(4) Pale ambapo mtu ambaye amehojiwa na afisa polisi hawezi kusoma taarifa au mahojiano au amekataa kusoma, au imeonekana kwa afisa polisi kutotaka kusoma taarifa hiyo wakati anaonyeshwa mtu huyo kulingana na kifungu kidogo cha (3), afisa polisi:–
(a) atamsomea taarifa hiyo au atasababisha mtu huyo asomewe taarifa hiyo;
(b) atamuuliza kama angependa kusahihisha au kuongeza chochote kwenye taarifa hiyo;
(c) atamruhusu mtu huyo kusahihisha , kubadilisha au kuongeza kwenye taarifa au kufanya masahihisho yoyote, mabadiliko au kuongeza kwenye taarifa ambayo atamuomba afisa polisi kufanya;
(d) atamtaka kusaini cheti mwisho wa kuchukua taarifa; na
(e) kuthibitisha na mkono wake, mwisho wa taarifa alichofanya kulingana na kifungu hiki kidogo.
Dhamana ya mashahidi
34. (1) Afisa polisi yeyote mwenye haki ya kutaka mahudhurio ya mtu yeyote kwa mujibu wa masharti yaliyopo kwenye kifungu cha 32 cha Sheria hii anaweza kumtaka mtu huyo kupata hati ya dhamana, katika namna inayohitajika, kuhudhuria na kutoa ushahidi mbele ya hakimu pale ambapo inahitajika kufanyika hivyo.
(2) Mtu yeyote ambaye anakiuka au anashindwa kukubaliana na mahitaji yaliyopo katika kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki atakuwa ametenda kosa.
Upekuzi na Maafisa Polisi Sheria Na. 9 ya 1985 kifungu cha 397; 5 ya 1993 Jedwali 397;5 ya 1993 Jedwali]
35. (1) Kama afisa polisi msimamizi wa kituo cha polisi anaridhika kwamba kuna sababu za msingi za kushuku kwamba kuna kjengo lolote, meli, boksi la mizigo, chombo cha kuwekea vitu au sehemu kuna:–
(a) kitu chochote kinachohusiana na kosa lililotendeka;
(b) kitu chochote kinachopelekea kuwa ni sababu za msingi kuamini kwamba itasaidia kama ushahidi katika kutendeka kwa kosa hilo;
(c) kitu chochote kinachopelelekea kuwa ni sababu za msingi kuamini kwamba kilikusudiwa kutumika kwa dhumuni la kutenda kosa lolote,
na afisa anaridhika kwamba ucheleweshwaji wowote utapelekea kuondolewa au kuharibiwa kwa kitu hicho, au ungehatarisha maisha au mali, anaweza kupekuwa au kutoa kibali kwa maandishi kwa afisa polisi yeyote wa chini yake cha kupekuwa jengo hilo, meli, boksi la mizigo, chombo cha kuwekea vitu, au sehemu kama itakavyokuwa.
(2) Pale mamlaka yoyote iliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) imetolewa, afisa polisi anayehusika, kwa haraka kama itakavyowezekana,
21
atatoa taarifa ya mamlaka, sababu zilizopelekea kutolewa, na matokeo ya upekuzi wowote uliofanyika kwa hakimu.
(3) Pale ambapo kitu chochote kimekamatwa kulingana na na mamlaka yaliyotajwa na kifungu kidogo cha (1), afisa aliyekamata kitu hicho atatoa risiti kudhibitisha kukamatwa kwa kitu hicho ikiwa na saini ya mwenye mali hizo, na saini za mashahidi wa upekuzi kama wapo.
(4) Masharti ya kifungu cha 38(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai* yanayohusiana na upekuzi, kama itakavyoweza kuwa, yatatumika katika upekuzi uliotajwa katika kipengele hiki
(5) Hakuna mashtaka dhidi ya mtu yoyote kwa kosa lililopo chini ya kifungu kidogo cha (4) litakalofunguliwa isipokuwa kwa kibali cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka. [kifungu cha 34]
Mamlaka ya kuchukua alama za vidole, picha n.k Sheria Na. 9 ya 1985 kifungu cha 397
36. (1) Afisa polisi yoyote msimamizi wa kituo cha polisi au afisa polisi yeyote anayechunguza kosa anaweza kuchukuwa au kusababisha kuchukuliwa kwa vipimo au alama za mikono, vidole, miguu au vidole vya miguu, au rekodi ya sauti au picha, mifano ya miandiko, ya mtu yeyote aliyetuhumiwa kwa kosa, labda mtu huyo yuko kihalali chini ya ulinzi wa polisi au vinginevyo pale ambapo vipimo hivyo, alama, rekodi, picha, au mifano, kama itakavyokuwa, kimsingi imeaminika kuwa lazima kufanya utambuzi wa mtu kuhusiana na , au kusaidia kama ushahidi katika kutendeka kwa kosa ambalo amewekwa chini ya ulinzi au kushtakiwa.
(2) Afisa polisi yoyote msimamizi wa kituo cha polisi au afisa polisi yeyote anayechunguza kosa anaweza kuchukuwa au kusababisha kuchukuliwa kwa vipimo au alama za mikono, vidole, miguu au vidole vya miguu, au rekodi ya sauti au picha, mifano ya miandiko, ya mtu yeyote aliyetuhumiwa kwa kosa, labda mtu huyo yuko kihalali chini ya ulinzi wa polisi au vinginevyo pale ambapo vipimo hivyo, alama, rekodi, picha, au mifano, kama itakavyokuwa, kimsingi imeaminika kuwa lazima katika kusaidia uchunguzi wa kosa.
(3) Hakuna mtu ambaye yuko chini ya ulinzi au ameshtakiwa lakini sio ulinzi halali, atakuwa na haki ya kukataa au kupinga kutoa vipimo vyake, alama, rekodi, picha au mfano wa mwandiko wake uliochukuliwa, na pale ambapo anakataa au kupinga, afisa polisi anayehusika anaweza kuchukuwa hatua za kutosha, ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu ya kiasi , kama itakavyokuwa muhimu katika kupata vipimo hivyo, alama, rekodi, picha au mifano, kama itakavyokuwa, kuchukuliwa.
(4) Mtu yeyote ambaye anakataa kutoa vipimo vyake, alama, rekodi, picha au mifano iliyochukuliwa kama inavyohitajika chini ya kifungu kidogo cha (1) na (2) ana hatia ya kosa na atahukumiwa kutoa fidia isiyozidi shillingi elfu kumi au kifungo kisichozidi miezi ishirini na nne au yote kwa pamoja fidia na kifungo.
(5) Kufuatia masharti yaliyoko katika kifungu kidogo cha (10), mtu ambaye ana vipimo, alama, rekodi, picha au mifano na kila mtu ambaye ana nakala ya vipimo, alama, rekodi, picha au mifano atavitelekeza:-
(a) katika kesi ya mtu ambaye yuko kisheria chini ya ulinzi katika
22
shitaka la kutenda kosa:-
(i) kama mashtaka ya mtu huyo hayaendelezwi; au
(ii) pale ambapo mashtaka yanaendelea lakini ameachiwa huru;
(b) katika kesi ya mtu ambaye ametajwa katika kifungu kidogo cha (2), kama vipimo hivyo, alama, rekodi, picha, au mifano, kama itakavyokuwa havihitajiki tena kwa dhumuni la kusaidia uchunguzi.
(6) Itaanzishwa sehemu itakayoidhinishwa na Waziri mwenye dhamana na uchunguzi wa kesi za jinai, ofisi itakayojulikana kama Ofisi ya Kumbukumbu ya Makosa ya Jinai kwa ajili ya kulinda, kulinganisha na, kuorodhesha fomu za alama za vidole.
(7) Ofisi ya Kumbukumbu ya Makosa ya Jinai, kulingana na usimamizi wa jumla wa Mrakibu Mkuu, itakuwa chini ya usimamizi wa afisa polisi mwandamizi, mwenye ujuzi katika kulinganisha alama za vidole, ambaye atateuliwa mara kwa mara na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa taarifa itakayotangazwa kwenye gazeti la Serikali.
(8) Fomu za alama za vidole zilizokamilika zitapatikana na kuhifadhiwa katika ofisi ya Kumbukumbu ya Makosa ya Jinai.
(9) Fomu zote za alama za vidole zitakuwa katika sampuli iliyokubalika.
(10) Bila kujali masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (5), itakuwa ni halali kisheria kuzuia kumbukumbu zote zilizopatikana kulingana na vifungu vidogo vya (1) na (2) vya kifungu hiki kulingana na mtu yeyote ambaye amri ya kuondolewa chini ya sheria ya Mji Mdogo (Uondoaji wa Watu Wasiohitajika au Amri ya Uondoaji chini ya Sheria ya Uondoaji wa Watu Wasiohitajika) imetolewa na kufutwa au kubatilishwa. [kifungu cha 35]
Uchunguzi wa kitabibu Sheria Na. 9 ya 1985 kifungu cha 397
37. (1) Hakimu anaweza, kwa maombi ya afisa polisi, kuruhusu afisa tabibu kumchunguza mtu aliyeko chini ya ulinzi kisheria kulingana na kosa au anaweza kuruhusu afisa tabibu kuchukuwa na kuchambua kielelezo chochote kutoka kwa mtu huyo kama ana sababu za kutosha za kuamini kwamba uchunguzi au uchambuzi ungesaidia kutoa ushahidi kuhusiana na kosa.
(2) Baada ya afisa tabibu kufanya uchunguzi na uchambuzi kama ilivyotajwa katika kifungu kidogo cha (1), atawasilisha ripoti iliyoandikwa kwa ajili hiyo mahakamani.
(3) Katika shauri lolote, mahakama inaweza kutoa amri kwamba mtu yeyote ambaye ni sehemu au shahidi katika shauri kufika kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu na mtu huyo atafika mwenyewe.
(4) Afisa tabibu baada ya kumchunguza mtu ambaye mahakama imetoa amri afike mwenyewe kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu kulingana na masharti ya kifungu kidogo cha (3) atawasilisha mahakamani ripoti ya maandishi kuhusiana na uchunguzi huo. [kifungu cha 35A]
Gwaride la utambuzi
38. (1) Afisa polisi yeyote msimamizi wa kituo cha polisi au afisa polisi yeyote anayepeleleza kosa anaweza kufanya gwaride la utambuzi kwa dhumuni la kuyakinisha kama shahidi anaweza kutambua mtu aliyetuhumiwa
23
kutenda kosa hilo.
(2) Afisa polisi yeyote msimamizi wa kituo cha polisi au afisa polisi yeyote anayepeleleza kosa anaweza kumtaka mtu yeyote ambaye kushiriki kwake ni lazima katika kupeleleza kosa afike na kushiriki katika gwaride la utambuzi.
(3) Hakuna mtu ambaye anahitajika kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) kuhudhuria na kushiriki katika gwaride la utambuzi atakuwa na haki ya kukataa au kupinga kuhudhuria na kushiriki katika gwaride la utambuzi.
(4) Mtu yeyote ambaye, bila sababu ya msingi anakataa kuhudhuria na kushiriki katika gwaride la utambuzi ana hatia ya kosa na atahukumiwa kwa kutoa faini isiyozidi shilingi elfu mbili au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote kwa pamoja faini na kifungo. [kifungu cha 35B]
Mamlaka ya kukagua leseni na kupekua magari
39. (1) Afisa polisi yeyote anaweza kusimamisha au kukamata mtu yeyote
(a) ambaye anamuona anafanya kitendo chochote au kitu; au
(b) ambaye anamuona anamiliki kitu chochote; au
(c) ambaye anamtuhumu kufanya tendo lolote au kitu au anamiliki kitu chochote ambacho kinahitaji leseni chini ya sheria yoyote ambayo inatumika kwa wakati huo na anaweza kuhitaji mtu huyo kuonyesha leseni hiyo, na anaweza kusimamisha na kupekuwa gari lolote ambalo ana sababu za kutosha kutuhumu kutumika katika kutenda kosa kinyume na sheria yoyote ambayo inatumika kwa wakati huo.
(2) Mtu yeyote ambaye ameshindwa kuonyesha leseni hiyo pale ambapo ameamriwa na polisi kufanya hivyo anaweza kukamatwa bila kibali, isipokuwa kama anatoa jina na anwani yake na kumridhisha afisa polisi kwamba atajibu wito wowote au mashtaka mengine ambayo yanaweza kutolewa dhidi yake.
(3) Mtu yeyote, ambaye ameshidwa kutii alama yoyote ya afisa polisi, inayomhitaji mtu huyo kusimamisha gari lolote, chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, au ambaye anamzuia afisa polisi yeyote katika kutekeleza majukumu yake chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo kilichotajwa atakuwa na hatia ya kosa , na afisa polisi yeyote anaweza kumkamata mtu huyo bila kibali, na anaweza kusababisha gari hiyo aliyoiona kuwa imetumika katika kutenda kosa kinyime na sheria yoyote inayotumika kupelekwa katika kituo cha polisi kilichoko karibu kuwekwa kizuizini mpaka litakapoachiliwa na afisa polisi msimamizi wa kituo hicho:
Isipokuwa kwamba kukamatwa huko hakutafanyika kama mtu huyo anatoa jina na anwani na kumridhisha afisa polisi huyo kama inavyoelezwa katika kifungu kidogo cha (2) cha kifungu hiki. [kifungu cha 36]
Jeshi kuweka amri kwenye barabara za umma.
40. (1) Itakuwa halali kisheria kwa Jeshi la Polisi kusimamia na kuongoza wendaji wa magari barabarani; kuonyesha njia ya mchepuko magari yote au baadhi katika barabara fulani, pale ambapo askari polisi msimamizi anaona inafaa kufanya hivyo kwa manufaa ya umma; kufunga mtaa wowote kwa dhumuni la kuzuia kupinga mashtaka ya umma kwa kupiga kelele au kuwepo
24
kwa wendaji wa magari katika mtaa fulani; kutoa amri na kuzuia kizuizi katika barabara za umma, mitaa, njia, sehemu za kutua ndege au sehemu zingine zozote maalum za utalii au sehemu ambayo umma inaweza kupatumia, au kufanyika kwa mikusanyiko au maandamano katika barabara za umma na mitaa, au jirani na sehemu za kuabudu wakati wa muda wa kuabudu, au kwa namna yoyote pale ambapo barabara yoyote , mtaa, njia au sehemu ya kutua ndege inaweza kuwa na msongamano au inaweza kuharibiwa.
(2) Kila mtu ambaye anapinga au anashidwa kutii amri yoyote halali inayotolewa na afisa polisi katika kutekeleza majukumu yake chini ya kifungu hiki atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kutoa fidia isiyozidi laki nne au kifungo cha miezi mitatu.
(3) Mtu yeyote ambaye anapinga au anashindwa kutii amri yoyote ya halali inayotolewa na afisa polisi katika kutekeleza majukumu yake yaliyoko chini ya kifungu hiki anaweza kukamatwa na afisa polisi yeyote bila kibali isipokuwa kama anatoa jina lake na anwani na vinginevyo anamridhisha afisa polisi huyo kwamba ataitikia/atajibu wito wowote au mashtaka mengine ambayo yanaweza kutolewa dhidi yake. [kifungu cha. 37]
Vizuizi vya barabara
41. (1) Bila kujali masharti ya sheria nyingine yoyote inayotumika, mrakibu msimamizi au afisa msimamizi wa polisi mwingine yeyote anaweza, kama ameona kuwa ni lazima kufanya hivyo kwa dhumuni la kutunza na kulinda sheria na amri au kwa kuzuia au kugundua kosa la jinai, kujenga au kuweka vizuizi katika barabara au upande wa barabara yoyote au mtaa au katika sehemu yoyote ya umma kwa namna ambayo anaweza kuona inafaa.
(2) Afisa polisi aliyeko katika sare anaweza kuchukua hatua zote za kutosha kuzuia gari lolote ambalo liliendeshwa siku za nyuma kwa kuweka vikwazo vyovyote na dereva yeyote wa gari lolote ambaye anashindwa kufuata alama yoyote ya afisa polisi ikimhitaji kusimamisha gari hilo kabla ya kufikia kikwazo hicho, atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kutoa fidia isiyozidi shilingi elfu moja au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja fidia na kifungo.
(3) Mtu yeyote ambaye anashindwa kufuata alama zozote kama ilivyotajwa hapo juu katika kifungu kidogo cha (2) anaweza kukamatwa na afisa polisi yeyote bila kibali.
(4) Hakuna afisa polisi atahukumiwa kwa upotevu au uharibifu wowote unaotokana na gari au kuumizwa kwa dereva au mmiliki mwingine yeyote wa gari hilo kufuatia kwa dereva wa gari hilo kushidwa kumtii afisa polisi yeyote anayetenda chini ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu hiki.
[kifungu cha. 38]
Mamlaka ya kudhibiti muziki na vitendo vya mikusanyiko n.k. Sheria Na 1 ya 1958
42. (1) Mrakibu mkuu au afisa polisi yeyote msimamizi anaweza, katika namna ambayo anaona inafaa, kutoa amri kwa madhumuni ya:-
(a) kudhibiti namna ambayo muziki unaweza kupigwa, au namna ambayo muziki au mazungumzo ya binadamu, au sauti nyingine yoyote inayoweza kupazwa, kutangazwa, kurusha habari au vinginevyo au kutengenezwa upya kwa namna ya bandia katika sehemu za umma;
25
kifungu cha 8
(b) kuelekeza vitendo vyote vya mikusanyiko na maandamano katika sehemu za umma, na kuainisha maeneo ambayo, na wakati ambao maandamano hayo yanaweza kupita, na anaweza, kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu, kutoa amri hizo kwa jinsi atakavyoona ni lazima au inafaa.
(2) Mtu yeyote amabaye anazembea au anakataa kufuata amri iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (1) atakuwa na hatia ya kutenda kosa na anaweza kukamatwa bila kibali na atahukumiwa kutoa faini isiyozidi shilingi mia tano au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja fidia na kifungo. [kifungu cha 39]
Mikusanyiko na maandamano ya hadhara Sheria Na. 1 ya 1958 kifungu cha 8; Sheria Na. 64 ya 1961 kifungu cha 5; 3 cha 1995 Jedwali
43. (1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.
(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.
(4) Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au mwendelezo wa mkusanyiko au maandamano katika hadhara/sehemu za umma ambayo yanaitishwa, kusanywa, kuundwa au andaliwa vinginevyo tofauti kulingana na taarifa chini ya kifungu kidogo cha (1) au kutokana na kwamba maelezo yaliyoainishwa na Waziri chini ya aya (c) ya kifungu kidogo cha (1) yamekiukwa au yanakiukwa , na anaweza, kwa dhumuni lolote lililotajwa, kutoa amri kama atakavyoona ni lazima au inafaa , ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya mkusanyiko wowote au maandamano kama ilivyotajwa hapo juu.
(5) Waziri anaweza, kwa amri, kutangaza kwamba masharti ya kifungu hiki hayatatumika katika mkusanyiko au maandamano yaliyoitishwa, kusanywa, kuundwa au kupangwa pasipokuwepo na sababu moja au zaidi au muungano wa sababu moja au zaidi kama itakavyoweza kuainishwa katika amri hiyo.
(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya
26
kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.
[kifungu cha 40]
Mamlaka ya kutawanya mikusanyiko na maandamano popote yanapofanyika Sheria Na. 3 ya 1995 Jedwali.
44. Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au kuendelea kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano yoyote katika sehemu yoyote ile kama, kwa mawazo ya afisa huyo anaona kufanyika au kuendelea kufanyika, kama inavyoweza kuwa, kwa mkusanyiko au maandamano hayo yanavunja amani au kuvuruga usalama wa umma au kulinda amani na amri, na anaweza, kwa manufaa ya umma, ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya kwa mkusanyiko huo au maandamano kama ilivyosemwa. [kifungu cha 41]
Wakati ambapo mikusanyiko au maandamano ni kinyume na SheriaNa. 1 ya1958 kifungu cha 8; Sheria Na. 3 ya 1995 Jedwali.
45. Mkusanyiko au maandamano yoyote ambayo watu watatu au zaidi wanaohudhuria au kuchukua nafasi wanazembea au kukataa kufuata amri yoyote ya kutawanywa iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 43 au kifungu cha 44, itahesabika kuwa mkusanyiko kinyume na sheria katika maana iliyopo katika kifungu cha 74 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*
[kifungu cha 42]
Adhabu Sheria Na. 1 ya 1958 kifungu cha 8; Sheria Na. 3 ya
1995
46. (1) Mtu yeyote ambaye:-
(a) anazembea au anakataa kufuata amri iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha 43 au kifungu cha 44; au
(b) anakiuka maelezo yoyote yakiyoainishwa na Waziri kulingana na aya ya (c) ya kifungu kidogo cha (1) cha 43,
atakuwa na hatia ya kutenda kosa na anaweza kukamatwa bila kibali na atahukumiwa kutoa fidia isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja fidia na kifungo.
(2) Kufuatia masharti yoyote ya amri yoyote yaliyopo katika kifungu kidogo cha (5) cha kifungu cha 43, pale ambapo mkusanyiko au maandamano yoyote katika eneo la umma yamefanyika, kusanyika, anzishwa au kupangwa vinginevyo tofauti na kulingana na kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 43:-
(a) mtu yeyote anayejihusisha katika kufanya, kukusanya, kuanzisha au kupanga mkusanyiko au maandamano hayo atakuwa na hatia ya kosa na anaweza kukamatwa bila kibali na atahukumiwa kutoa fidia isiyozidi shilingi laki mbili au kifungo kisichozidi kipindi cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja fidia na kifungo;
(b) Kila mtu anayehudhuria mkusanyiko huo au anayejihusisha katika maandamano hayo, ambaye anajua au ana sababu za kuamini kwamba mkusanyiko au maandamano hayo yamefanyika, kusanywa, anzishwa au kupangwa vinginevyo tofauti kulingana na masharti yaliyopo katika kifungu kidogo (1) cha kifungu cha 43, atakuwa na hatia ya kosa na anaweza kukamatwa bila kibali na atahukumiwa kutoa fidia
27
isiyozidi shilingi laki moja au adhabu ya kifungo kisichozidi miezi sita au adhabu zote kwa pamoja fidia na kifungo .
[kifungu cha. 43]
SEHEMU YA TANO
MALI ZISIZODAIWA
Mpangilio wa mali zisizodaiwa Sheria Na.1 ya 1958
47. (1) Itakuwa ni wajibu wa kila afisa polisi kuorodhesha mali zote zinazohamishika zisizodaiwa na kutoa orodha au maelezo yanayohusiana na mali hizo kwa hakimu.
(2) Kama mali hiyo sio fedha au mali ambayo haiwezi kuharibika haraka au mali ambayo kuuzwa kwa haraka, kungeweza, kwa maoni yake, kuwa ni kwa faida ya mmiliki, hakimu ataweka kizuizini au atatoa amri ya kuweka kizuizini kwa mali hiyo na atasababisha taarifa kutumwa katika sehemu ya wazi katika mahakama yake na katika vituo vya polisi vilivyopo ndani ya mamlaka yake kuonyesha mali hiyo na kumtaka mtu yeyote ambaye ana madai ya mali hiyo kuwepo mahakamani na kudhibitisha madai yake ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe ya taarifa hiyo. Iwapo hakimu ana maoni kwamba thamani ya mali hiyo ni wazi inazidi shilingi hamsini, pia atasababisha taarifa ya namna ileile kutangazwa katika Gazeti la Serikali, tarehe ambayo mtu yeyote anatakiwa kudhibitisha madai yake kuhusiana na mali hiyo kuwa ni tarehe ileile kama ilivyoelekezwa na hakimu katika taarifa aliyosababisha kutangazwa kienyeji.
(3) Kama hakuna mtu atakayejitokeza kudai mali hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe ya kutangazwa, mali hiyo inaweza kuuzwa au, kama hakimu anaona inafaa, inaweza kuharibiwa kwa amri ya hakimu, na baada ya kumalizika kuuzwa au kuharibiwa mali hiyo, haki ya kufungua mashtaka kwa ajili ya kulipwa mali hiyo haitakuwepo:
Isipokuwa kwamba kama mali hiyo ni silaha au risasi hakimu anaweza kutoa amri kwamba inaweza kuharibiwa kwa namna ambayo Mrakibu Mkuu anaweza kuelekeza.
(4) Mapato ya mauzo ya mali hiyo yatagawanywa katika namna ifuatayo:-
(a) nusu italipwa kwenye deni la Mfuko wa Tuzo wa Polisi;
(b) kiasi kilichobaki nusu kama hakimu atakavyoelekeza italipwa kwa aliyetafuta mali hiyo; na
(c) kiasi kilichobaki kitalipwa katika mapato ya jumla ya Jamhuri ya Muungano
(5) Iwapo hakimu anaona kwamba mali hiyo inatakiwa haraka au ina asili ya kuharibika au kuuzwa haraka ingekuwa kwa manufaa ya mwenye mali hakimu atazuia au atatoa amri ya kuzuia na anaweza kwa wakati wowote kuamuru kuuzwa bila ya taarifa iliyoelezwa katika kifungu kidogo cha (2) kutolewa kabla ya kuuzwa au, kama anafikiri inafaa kufanya hivyo, anaweza kutoa amri iharibiwe. Baada ya kumalizika kuuzwa mali hiyo au kuharibiwa chini ya kifungu hiki kidogo haki ya kufungua mashtaka kwa ajili ya kupata tena mali iliyouzwa au kuharibiwa haitakuwepo.
28
[kifungu cha (5A)]
(6) Mapato ya mauzo hayo yatakuwa chini ya ulinzi kama hakimu atakavyoweza kuelekeza na hakimu baada ya mauzo hayo atahakikisha taarifa ya mauzo hayo inatumwa mara moja kama ilivyoelezwa katika kifungu kidogo cha (2) ikielezea mali iliyouzwa na ikimhitaji mtu yeyote ambaye anaweza kudai kwenye mapato ya mauzo hayo kujitokeza na kuanzisha madai yake ndani ya miezi sita kuanzia tarehe ya taarifa hiyo. [kifungu cha (5B)]
(7) Mapato ya mauzo hayo yatalipwa kwa mtu ambaye ameanzisha madai yake. Baada ya miezi sita kumalizika kuanzia tarehe ya taarifa hiyo, kama hakuna mtu atakayeanzisha madai yake, haki ya kuanzisha mashtaka kwa ajili ya kupata tena mapato hayo haitakuwepo, na mapato hayo yatashughulikiwa kulingana na masharti ya kifungu kidogo cha (4).
[kifungu cha (5C)]
(8) Pale ambapo mali isiyodaiwa inayohamishika inakuwa na fedha itashughulikiwa kwa hatua zote kama vile yalikuwa ni mapato ya mauzo yaliyoamriwa kwa mujibu wa masharti ya vifungu vidogo vya (8) na (9).
[kifungu cha 44]
SEHEMU YA SITA
MASHTAKA DHIDI YA MAAFISA POLISI
(vifungu vya 48-49)
Kutokuwajibika kisheria kwa kitendo kilichofanyika chini ya mamlaka ya hati.
48. (1) Pale ambapo utetezi wa kesi yoyote iliyofunguliwa dhidi ya afisa polisi ni kwamba kitendo kinacholalamikiwa kilifanyika kufuatia hati inayodaiwa kutolewa na jaji, hakimu au mlinzi wa amani, baada ya kutolewa kwa hati yenye saini ya hakimu au mlinzi wa amani mahakama ataikubali hati hiyo kama ushahidi wa kwanza alioufanya, na baada ya kudhibitisha kwamba kitendo kinacholalamikiwa kilifanyika kulingana na hati hiyo, hakimu atatoa hukumu kwa manufaa ya askari polisi huyo.
(2) Hakuna udhibitisho wa saini ya hakimu au mlinzi wa amani utahitajika isipokuwa mahakama ina sababu ya kuwa na wasiwasi kuhusu uhalali wa hati hiyo; na pale ambapo itadhibitishwa kwamba saini hiyo sio halali, hukumu itatolewa kwa manufaa ya afisa polisi huyo kama imedhibitishwa kwamba, muda ambao inalalamikiwa kwamba kitendo kimefanyika, anaamini kutokana na sababu za kutosha kwamba saini hiyo ilikuwa halali. [kifungu cha. 45]
Mshahara wa maafisa polisi fulani kutokukamatwa kisheria kwa ajili ya pesa zilizokopwa au bidhaa zilizogawanywa.
49. Hakuna mshahara au marupurupu yanayolipwa kwa mwanachama yeyote wa Jeshi wa daraja la chini ya mrakibu yatapaswa kukamatwa, kunyang’anywa au kukatwa kodi kwa ajili ya deni au madai ya fedha yoyote iliyokopwa na afisa huyo au bidhaa zilizogawanywa kwake au kwa mtu yeyote badala yake wakati akiwa mwanachama wa Jeshi la Polisi.
[kifungu cha 46]
29
SEHEMU YA SABA
NIDHAMU (kifungu cha 50-65)
Makosa dhidi ya nidhamu
50. (1) Afisa yeyote wa Jeshi la Polisi wa daraja la mrakibu au chini ya daraja la mrakibu ambaye:-
(a) anashawishi au anajaribu kushawishi, anasababisha au anajaribu kusababisha, au anasaidia, afisa polisi yeyote kutelekeza, au kuwa na ufahamu na utekelezaji wowote au utelekezaji uliokusudiwa, bila ya kuchelewa, kutoa taarifa kwa afisa wa daraja la juu yake;
(b) anagoma au anatumia au anatumia nguvu dhidi ya afisa wa cheo cha juu;
(c) anatumia vitisho au lugha ya ukaidi kwa afisa wa daraja la juu yake;
(d) ana hatia ya vitendo vya ukaidi;
(e) anasababisha usumbufu katika kituo chochote cha polisi au kambi ya jeshi,
(f) hana utii katika maandishi, vitendo au mwenendo kwa afisa wa daraja la juu yake;
(g) anakataa kutii amri halali ya afisa wa daraja la juu yake;
(h) anashindwa kufuata na amri yoyote halali iliyotolewa na afisa wa daraja la juu yake;
(i) anajisababishia mwenyewe kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya ulevi;
(j) anakunywa pombe kali wakati akiwa kazini;
(k) amelewa akiwa akizini, au katika laini za polisi , kambi ya jeshi, au kituo au akiwa katika sare;
(l) anakosa kazini bila likizo;
(m) analala wakati akiwa kazini;
(n) anaondoka katika kituo chake kabla hajapokelewa isipokuwa kwenye jambo jipya la mtuhumiwa yeyote ambaye ana jukumu la kumkamata;
(o) akiwa chini ya ulinzi au kizuizini anaacha au anatoroka kabla ya kuachiwa huru na mamlaka husika;
(p) anazembea au anakataa kusaidia katika kumkamata mwanachama yeyote
(q) kwa uzembe anaruhusu mfungwa yeyote kutoroka ambaye amemtuhumu au ni wajibu kumhifadhi au kumlinda;
(r) anatoa au anatumia nguvu binafsi zisizoidhiniwa kumfanyia vibaya mtu yeyote aliyeko chini ya ulinzi wake;
(s) ana hatia ya woga;
(t) anaondoa silaha yoyote bila idhini au sababu ya kutosha;
(u) bila sababu ya kutosha anashidwa kuhudhuria katika gwaride lolote lililoteuliwa na afisa wa daraa la juu yake;
(v) weka rahani, uza, kupoteza kwa uzembe, kujiweka mbali, kuharibu kwa makusudi au kushindwa kutoa taarifa kuhusu
30
uharibifu kwenye jeshi lolote, risasi, vifaa vyote vya askari isipokuwa mavazi na silaha, sare au kitu kingine kilichopelekwa kwake au mali yoyote iliyokuwa chini ya usimamizi wake;
(w) anamiliki isiyokuwa halali mali yoyote ya umma, au mali yoyote ya mwanachama mwingine yeyote wa Jeshi, au mali ya mfungwa yeyote;
(x) anafanya kosa lolote la unyang’anyi au kutokuzuia uharibibu wa mali;
(y) anakubali au anachukuwa rushwa au bakshishi;
(z) ni mvivu au mzembe katika kutekeleza majukumu yake;
(aa) ni mkoo, sio msikivu, mstaarabu au mgomvi;
(bb) anakwenda kazini katika hali ya uchafu au silaha,mavazi au vifaa viko katika hali ya uchafu;
(cc) bila ya mamlaka anaweka wazi au kusambaza taarifa yoyote inayohusiana na upelelezi au polisi wengine kuhusiana na mambo ya kitengo;
(dd) anatengeneza au anasaini taarifa yoyote ya uongo katika kumbukumbu yoyote ya kiofisi au nyaraka;
(ee) anatengeneza au anajiunga katika kutengeneza madai yasiyojulikana;
(ff) mtegaji au anajisingizia au anajisababishia kwa makusudi ugonjwa wowote au udhaifu;
(gg) ana hatia ya mwenendo mbaya, au kutotii kwa makusudi, iwe hospitalini au popote, amri yoyote, na hivyo kusababisha au kuongeza ugonjwa au udhaifu au kuchelewesha kupona;
(hh) ameambukizwa ugonjwa wa zinaa au ugonjwa mwingine na kushindwa kutoa taarifa mapema kwa afisa tabibu wa Serikali kwa matibabu;
(ii) ana madeni ndani na nje ya Jeshi ambayo hawezi kulipa;
(jj) bila ya mamlaka husika analipisha kutoka kwa mtu yeyote, ubebaji,upakuaji au utumiaji;
(kk) anakataa msindikizaji ambae wajibu wake ni kumkamata au kumsimamia;
(ll) baada ya kutiwa hatiani kuhalali, anavunja laini za polisi, kambi au makazi;
(mm) anatoa taarifa yoyote ya uongo wakati wa kujiunga na Jeshi;
(nn) anakataa au anazembea kuandaa au kutuma ripoti yoyote au marejesho ambapo ni jukumu lake kuandaa au kutuma;
(oo) kwa makusudi anatoa mashtaka ya uongo dhidi ya mwanachama wa Jeshi;
(pp) katika kutoa malalamiko dhidi ya mwanachama yeyote wa Jeshi, akiwa anajua anatoa taarifa ya uongo inayoadhiri tabia ya mwanachama huyo au akiwa anajua na kwa kudhamiria anazuia taarifa yoyote ya kweli;
(qq) [Imefutwa.]
(rr) anajihusisha bila mamlaka katika ajira yoyote au ofisi tofauti
31
na kazi zake za kipolisi;
(ss) anakuwa askari wa polisi wa usalama kwa mtu yeyote au anajihusisha na shughuli yoyote ya mkopo na afisa polisi yeyote bila ya ruhusa ya maandishi ya Inspekta Jenerali Mkuu;
(tt) kama amehitajika na afisa wa gazeti la serikali kutoa taarifa nzima na ya kweli kuhusiana na hali yake ya kifedha na akashindwa kufanya hivyo;
(uu) kutotii kwa kudhamiria kanuni au amri ya jeshi;
(vv) ana hatia ya kitendo chochote, mwenendo, kutokutii amri au uzembe unaoathiri amani au nidhamu ya Jeshi, au katika kukiuka majukumu katika ofisi yake, au mienendo yoyote mibaya kama mwanachama wa Jeshi ambayo hayajatajwa hapo juu,
atahesabika kutenda kosa dhidi ya nidhamu, na atapata adhabu hiyo kutegemeana na kiwango na asili ya kosa, kama itakavyoweza kutolewa kulingana na masharti ya Sheria hii.
(2) afisa yeyote aliyeandikishwa kwenye gazeti la Serikali, inspekta au afisa asiyekuwa na cheo anaweza kukamata au kuamuru kukamatwa bila kibali cha afisa polisi yeyote (ambaye siyo afisa wa cheo chake au cheo cha juu yake) au mfuatiliaji ambaye ameshtakiwa kwa kosa chini ya kufungu hiki; na afisa polisi yeyote anaweza, baada ya kupata amri hiyo kama ilivyosemwa hapo juu, kumkamata mtuhumiwa huyo bila idhini na atampeleka mara moja kwa afisa msimamzi wa polisi, ambaye atapelekea kesi kusikilizwa bila kucheleweshwa na anaweza kuamuru mahabusu ya mtu aliyetuhumiwa kuwa chini ya ulinzi kwa muda mrefu kama atakavyokuwa muhimu kutosha.
[kifungu cha 47]
Mamlaka ya afisa kufanya uchunguzi
51. Pale ambapo shtaka lolote limeletwa sehemu yoyote chini ya kifungu cha 50, afisa msimamizi wa polisi wa sehemu hiyo, kama ni afisa aliyeandikishwa katika gazeti la serikali, au pale ambapo afisa huyo hayupo, afisa tawala yeyote mwenye uwezo na mamlaka ya hakimu wa wilaya katika sehemu hiyo, anaweza kufanya uchunguzi kuhusu ukweli wa shtaka hilo na anaweza kumwachia huru mtuhumiwa au kutoa adhabu kulingana na kifungu cha 53 au kupeleka kesi kwa afisa mwandamizi kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 52. [kifungu cha 48]
Taratibu za uchunguzi Na. 1 ya 1958 kifungu cha 90
52. (1) Katika kesi yoyote pale ambapo afisa anayefanya uchunguzi katika shtaka lolote chini ya kifungu cha 50:-
(a) anafikiria kwamba kosa ambalo mtuhumiwa amefanya, kwa sababu ya uzito wake au kwa sababu ya makosa ya nyuma au kwa sababu nyingine yoyote hataweza kuadhibiwa vya kutosha kwa adhabu yoyote ambayo afisa huyo amepewa mamlaka ya kuitoa; au
(b) ameelekezwa na afisa wa daraja la juu yake kuipeleka/kuirejesha kesi hiyo,
Afisa huyo atatofautiana kutoa adhabu na ataipeleka kesi kwa inspekta msimamizi wa kituo cha polisi.
32
(2) Inspekta Msimamizi wa kituo cha polisi ambaye kesi yoyote imepelekwa kwake chini ya kifungu kidogo cha (1):-
(a) anaweza kuirudisha kesi kwa afisa ambaye ilipelekwa kwake kwa kusikilizwa na kutoa maamuzi au kuchukuwa ushahidi zaidi; au
(b) anaweza kufanya uchunguzi wa kesi ama kwa kuchukua ushahidi zaidi mwenyewe au bila kuchukua au afisa polisi ambaye kesi ilipelekwa kwake, na kutoa adhabu.
(c) anaweza kuipeleka kesi hiyo kwa Kamishna Msaidizi anayefaa; au
(d) pale ambapo inspekta msimamizi huyo hayuko chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Kamishna Msaidizi, anaweza kuipeleka kesi hiyo kwa Inspekta Generali Mkuu.
(3) Kamishna Msaidizi ambaye kesi imepelekwa kwake chini ya kifungu kidogo cha (2):-
(a) anaweza kuipeleka kesi hiyo kwa msimamizi wa polisi, au kuipeleka kwa afisa polisi mwingine yeyote , kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa maamuzi au kupata ushahidi mwingine zaidi; au
(b) anaweza mwenyewe kufanya uchunguzi wa kesi, iwe kwa kuchukua au bila kuchukua ushahidi na afisa polisi yeyote kama ilivyotajwa katika aya ya (a), na kutoa adhabu; au
(c) anaweza kuipeleka kesi hiyo kwa Inspekta Jenerali Mkuu; au
(d) anaweza kuamuru mshtakiwa kupelekwa mbele ya hakimu ashughulikiwe kama ilivyoelezwa katika kifungu kidogo cha (5) cha kifungu hiki.
(4) Inspekta Jenerali Mkuu ambaye kesi yoyote imepelekwa kwake chini ya kifungu kidogo cha (2) au (3):-
(a) anaweza kuirudisha kesi hiyo kwa Kamishna msaidizi, au kuipeleka kwa afisa polisi yeyote, kwa kusikilizwa na kutoa maamuzi au kuchukuwa ushahidi zaidi; au
(b) anaweza mwenyewe kufanya uchunguzi wa kesi, iwe kwa kuchukua au bila kuchukua ushahidi zaidi na afisa polisi yeyote kama ilivyotajwa katika aya ya (a), na kutoa adhabu; au
(c) anaweza kuamuru mshtakiwa kupelekwa mbele ya hakimu ashughulikiwe kama ilivyoelezwa katika kifungu kidogo cha (5) cha kifungu hiki.
(5) Pale ambapo mshtakiwa amepelekwa mbele ya hakimu kama ilivyoelezwa kabla katika kifungu hiki atasikilizwa chini ya sheria hii katika namna iliyo sawa kama vile alikuwa ameshtakiwa kwa kosa lolote katika mahakama ya chini na atakuwa na hatia kwa kosa lolote lililotajwa katika kifungu cha 50 kwa faini isiyozidi malipo ya miezi mitatu au kwa kifungo kisichosidi miezi sita:
Alimradi kwamba hakuna mashtaka yatakayochukuliwa dhidi ya afisa polisi yeyote mbele ya hakimu kutokana na kosa lolote ambalo tayari ameshapewa adhabu chini ya kifungu cha 53 au 54 ya Sheria hii.
(6) Amri yoyote inayodaiwa kuwa amri ya Inspekta Jenerali Mkuu au Kamishna Msaidizi iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au (4) ya kifungu hiki itakubalika kama ushahidi wa kwanza wa sheria hii , na hakuna udhibitisho wa sahihi ya Inspekta Jenerali Mkuu au Kamishna Msaidizi
33
utakaohitajika katika amri yoyote hiyo isipokuwa pale ambapo mahakama ina sababu ya kutia shaka uhalali wa sahihi hiyo. [kifungu cha 49]
Adhabu kwa makosa dhidi ya nidhamu sheria. Na. 1 ya 1958 kifungu cha 11
53. (1) Kutokana na hatia yoyote ya kosa dhidi ya adhabu, afisa polisi yeyote mwenye mamlaka ya kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 51 anaweza kutoa adhabu moja au zaidi katika hizi zifuatazo:-
(a) kama ni mrakibu, onyo;
(b) kama ni afisa asiyekuwa na cheo:-
(i) onyo;
(ii) karipio;
(iii) faini isiyozidi shilingi elfu kumi;
(c) kama ni polisi wa daraja la chini:-
(i) onyo;
(ii) kufungiwa kwenye kota za polisi kwa kipindi kisichozidi siku kumi na nne;
(iii) ulinzi wa ziada, kazi za sulubu au kazi nyingine;
(iv) faini isiyozidi shilingi elfu kumi;
(v) kuwekwa kizuizini kwa kipindi kisichozidi siku saba;
(d) kama ni wafuatiliaji:-
(i) onyo;
(ii) faini isiyozidi shilingi elfu kumi;
(iii) kusitisha nyongeza;
(iii) kupunguza kiwango kidogo cha malipo;
(iv) kuachishwa kazi.
Katika muda wowote kabla ya adhabu yoyote iliyotolewa kutekelezwa chini ya kifungu hiki kidogo inaweza kubadilishwa na msimamizi wa polisi ambaye afisa anayetoa adhabu ni wa daraja la chini yake, au na Kamishna au Kamishna Msaidizi ambaye Kamishna amemkaimu madaraka yake kwa maandishi chini ya kifungu hiki:
Alimradi kwamba hakuna adhabu itakayoongezwa isipokuwa mshtakiwa alishapewa nafasi ya kuonyesha sababu kwa nini adhabu hiyo isibadilishwe.
(2) Kamishna Msaidizi au inspekta msimamizi wa polisi ambaye yamepelekwa kwake mashtaka kutokana na kosa dhidi ya nidhamu anaweza kutoa adhabu moja au zaidi kati ya adhabu zilizoorodheshwa katika kifungu kidogo cha (1) au adhabu moja au zaidi kati ya adhabu zifuatazo:-
(a) kama ni Inspekta:-
(i) karipio kali;
(ii) faini isiyozidi mshahara wa mwezi mmoja;
(iii) kushushwa cheo;
(iv) kusitisha nyongeza;
(b) kama ni afisa wa Jeshi wa daraja la chini ya inspekta
msaidizi:-
(i) faini isiyozidi mshahara wa mwezi mmoja;
(ii) kuachishwa kazi;
(iii) kuwekwa kizuizini kwa kipindi kisichozidi siku
kumi na nne;
34
(iv) kushushwa cheo;
(v) kusitisha nyongeza.
[kifungu 50]
Mamlaka maalumu ya Inspekta Jenerali Mkuu
54. (1) Inspekta Jenerali Mkuu anaweza, kutokana na mashtaka yoyote ya kosa dhidi ya nidhamu yaliyopelekwa kwake chini ya kifungu cha 51, kufanya uchunguzi na kutoa adhabu moja au zaidi ya adhabu zilizoorodheshwa katika kifungu cha 53 au adhabu moja au zaidi kati ya adhabu zifuatazo:-
(a) kama ni Inspekta:-
(i) karipio kali;
(ii) faini isiyozidi mshahara wa mwezi mmoja;
(iii) kushushwa cheo;
(iv) kusitisha malipo ya nyongeza;
(b) kama ni afisa yeyote wa Jeshi mwenye daraja la chini ya
Inspekta Msaidizi:-
(i) faini isiyozidi mshahara wa mwezi mmoja;
(ii) kufukuzwa;
(iii) kudhibitiwa nidhamu kwa kipindi kisichozidi siku kumi
na nne;
(iv) kushushwa cheo;
(v) kusitisha malipo ya nyongeza.
(2) Kama ni inspekta, Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kutoa mapendekezo kwa Waziri kufukuzwa kwa afisa huyo na Waziri anaweza kutokana na mapendekezo hayo kumfukuza afisa anayehusika.
(3) Kamishna anaweza kwa maandishi kukaimisha mamlaka yak echini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki kwa Kamishna Msaidizi:
Ilimradi kwamba adhabu yoyote ya kufukuzwa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi huyo lazima yawe yamepitishwa na Kamishna.
[kifungu cha 51]
Mamlaka ya afisa anayefanya uchunguzi
55. (1) Afisa yeyote aliyepewa mamlaka chini ya Sehemu hii kufanya uchunguzi katika shtaka au kesi yoyote atakuwa na mamlaka ya kuwaita na kuwachunguza mashahidi na kuhitaji utoaji wa nyaraka zote zinazohusiana na uchunguzi huo na anaweza kuahirisha kusikilizwa kwa kesi mara kwa mara kutokana na masharti kama atakavyoona inafaa, na mamlaka ya kumuweka mtuhumiwa chini ya ulinzi mpaka siku ya kusikilizwa. Mashtaka yote yatarekodiwa katika namna ambayo inaweza kuhitajika na kanuni au masharti yaliyotengenezwa chini ya Sheria hii.
(2) Mtu yeyote aliyeitwa kama shahidi chini ya masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki ambaye ameshindwa kuhudhuria kwa wakati na sehemu iliyotajwa kwenye wito au kuahirishwa kokote, au amekataa kujibu swali lolote aliloulizwa ipasavyo, atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kutoa faini isiyozidi shilingi mia au kwa kifungo cha mwezi mmoja:
Alimradi kwamba hakuna shahidi atalazimika kujibu swali lolote ambalo linaweza kupelekea kuwa hatarini au kumsababisha kuwa na hatia kwa utwaliwaji wa mali au adhabu yoyote.
[kifungu cha. 52]
35
Rufaa dhidi ya adhabu ya makosa dhidi ya nidhamu
56. (1) Mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye adhabu yoyote imetolewa kwake chini ya kifungu cha 53, anaweza kukata rufaa dhidi ya adhabu kwa mrakibu msimamizi wa polisi, na kama ni rufaa ya kwanza au ya pili, kwa Kamishna Msaidizi, na kama ni adhabu yoyote tofauti na onyo, ulinzi wa ziada, kazi za sulubu au kazi nyingine, baadaye kwa Kamishna, na kutokana na jinsi ilivyoeleza katika kifungu kidogo cha (2), maamuzi ya afisa mwandamizi aliyepewa mamlaka ya kushughulikia rufaa yatakuwa ya mwisho.
(2) Afisa yeyote wa Jeshi ambaye amepewa adhabu na Kamishna chini ya kifungu cha 54 kwa kufukuzwa au ambaye adhabu ya kuondolewa imedhibitishwa na Kamishna chini ya kifungu cha 54 kilichotajwa anaweza, ndani ya siku saba baada ya kupata uamuzi au udhibitisho wa kamishna, kukata rufaa kwa Waziri ambaye uamuzi wake utakuwa wa mwisho.
(3) Katika rufaa hiyo kama ilivyotajwa katika kifungu kidogo cha (1), Kamishna au afisa mwingine anayesikiliza rufaa atakuwa na mamlaka ya:-
(a) kurudisha mashtaka kwa ajili ya kuchukua ushahidi zaidi;
(b) iwe ushahidi zaidi umechukuliwa au la, kutupilia mbali mashtaka na kusikiliza upya kesi mwenyewe upya au kuamuru kesi hiyo isikilizwe upya na afisa mwingine katika namna iliyo sawa kama vile kesi hiyo imeshughulikiwa chini ya kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 52;
(c) kubatilisha au kutofautiana na ugunduzi wowote;
(d) kufuta, kuongeza au kutofautiana na adhabu yoyote.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake chini ya aya ya (d) ya kifungu kidogo cha (3) cha kifungu hiki Kamishna au afisa mwingine anayesikiliza rufaa anaweza kutoa adhabu yoyote au adhabu ambazo angekwisha zitoa chini ya kifungu cha 54 kama angezisikiliza kesi mwenyewe: [kifungu cha 53]
Kuzuiwa wakati wa uchunguzi na kusimamishwa Ord. Na. 22 ya 1955 kifungu cha 9
57. (1) Kamishna au, kutokana na mwanachama yeyote wa Jeshi chini ya utawala wake, Kamishna Msaidizi, Inspekta msaidizi wa polisi, au afisa msimamizi wa polisi, anaweza kumzuia kazi afisa yeyote wa Jeshi tofauti na mwanachama aliyeandikishwa katika gazeti la serikali, ambaye uchunguzi wake unaendelea chini ya masharti ya kifungu cha 51 au kifungu cha 52, au ambaye ameshtakiwa mahakama yoyote kutokana na kosa lolote chini ya Sheria hii au Sheria nyingine yoyote:
Alimradi kwamba amri ya kuzuiwa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi au Inspekta Msaidizi wa polisi au afisa msimamizi wa polisi lazima iwasilishwe kwa Kamishna bila kuchelewa kwa ajili ya kutoa idhini yake.
(2) Kamishna anaweza kwa hiyari yake kumsimamisha kazi mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye amri ya kufukuzwa ilishatolewa na ambaye amekata rufaa kupinga amri hiyo au mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye amehukumiwa kifungo na mahakama yoyote kutokana na kosa lolote, chini ya Sheria hii au vinginevyo, na ambaye amekata rufaa dhidi ya adhabu hiyo. [kifungu cha 54]
Afisa aliyezuiwa au
58. (1) Afisa wa Jeshi kwa sababu ya kuzuiliwa au kusimamishwa kazi
36
kusimamishwa kuendelea kuwa afisa polisi
hatakoma kuendelea kuwa mwanachama wa Jeshi. Katika kipindi hicho cha kuzuiliwa au kusimamishwa mamlaka, wajibu na marupurupu aliyopewa kama mwanachama wa Jeshi hayatatumika, lakini ataendelea kuwajibika na majukumu, nidhamu na adhabu na katika mamlaka hiyohiyo kama vile hakuwahi kuzuiliwa au kusimamishwa.
(2) Hakuna malipo yatakayoongezeka au kutakiwa kulipwa kwa mwanachama yeyote wa Jeshi kutokana na kipindi cha kusimamishwa isipokuwa kama Waziri atakavyoweka uwiano.
(3) Bila kujali kitu chochote kilichopo katika kifungu kidogo cha (2) na (3) cha kifungu hiki, kama mashtaka dhidi ya mwanachama yeyote wa Jeshi hayakupelekea kufukuzwa kwake au kupewa adhabu nyingine yoyote, atakuwa na haki ya mshahara wote ambao angekuwa anapata kama hakuzuiliwa au kusimamishwa kazi. [kifungu cha 55]
Kufukuzwa na kushushwa cheo kwa maafisa polisi baada ya kuhukumiwa.
59. Kamishna anaweza kumshusha cheo, daraja au anaweza kumfukuza mjumbe yeyote wa Jeshi kutoka Jeshini tofauti na afisa aliyeandikishwa kwenye gazeti ambaye ameshahukumiwa na mahakama yoyote kwa kosa, chini ya Sheria hii au vinginevyo, isipokuwa mwanachama huyo wa Jeshi amefanikiwa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. [kifungu cha 56]
Faini kupatikana kwa kuzuia malipo.
60. (1) Faini zote zinatozwa kwa mwanachama wa Jeshi kutokana na makosa chini ya Sheria hii au kanuni zozote zilizotengenezwa zinaweza kupatikana kwa kuzuia malipo ya mhalifu wakati wa kutenda kosa hilo na baadaye malipo yatakayoongezeka.
(2) Kiasi kinachozuiliwa kutokana na faini au kwa sababu nyingine yoyote yaliyoidhinishwa na Sheria hii au na kanuni zilizotengenezwa kwa ajili hiyo itakuwa ni hiyari ya afisa ambaye faini imetozwa, kufuatana na maagizo ya mrakibu msimamizi wa polisi au Kamishna Msaidizi ambaye yuko chini yake, au Kamishna, lakini katika kesi yoyote hatazidisha nusu ya mshahara wa mhalifu; na pale ambapo kuna amri zaidi ya moja ya kuzuia malipo dhidi ya mtu mmoja ni mshahara wake tu utazuiliwa kama atakavyobaki na angalau nusu ya mshahara wake.
(3) Pale ambapo amri zaidi ya moja ya kuzuiliwa zimetolewa kwa mtu huyohuyo, amri zilizotolewa mwishoni, kama ni lazima, zitaahirishwa kuhusu utekelezaji wake mpaka amri zilizotolewa mwanzoni zimeondolewa.
[kifungu cha 57]
Hasara ya au uharibifu wa silaha au vifaa vyote vya askari kulipwa kwa kuzuia malipo.
61. Kama afisa yeyote wa Jeshi cheo cha inspekta au cheo cha chini anaweka rehani, anauza, poteza kwa uzembe, anajiweka mbali na au kwa kudhamiria au kwa uzembe anaharibu silaha yoyote, risasi, vifaa vya askari, sare au makala yoyote aliyopewa, au kifaa chochote kilichowekwa chini ya usimamizi wake, anaweza, kama nyongeza ya au kulingana na adhabu nyingine yoyote, kuamriwa kulipa gharama yote au kiasi chochote kutokana na upotevu au uharibifu na kiasi hicho kinaweza kupatikana kwa kuzuia malipo yake. [kifungu cha 58]
Kutokuwepo na
62. Hakuna malipo yatakayolipwa kwa mwanachama yeyote wa Jeshi wa
37
malipo kwa kukosa kazini bila likizo, kifungo au kuwekwa kizuizini Sheria. Na. 1 ya 1958 kifungu cha 13
cheo cha chini ya mrakibu msaidizi yanayotokana na kipindi chochote ambacho hakuwepo kazini bila ya likizo au anatumikia adhabu yoyote ya kifungo au kinidhamu kwa kosa lolote dhidi ya nidhamu au kwa kosa la aina yoyote:
Aimradi kwamba kwa namna yoyote Kamishna anaweza, kwa hiyari yake kuidhinisha malipo yenye uwiano, yasiyozidi nusu kama atakavyoona inafaa. [kifungu cha 59]
Sehemu ya kuwafunga wahalifu Sheria Na. 64 ya 1961 s. 6; Gzt Na. 73 la 1965
63. Mwanachama yeyote wa Jeshi aliyekamatwa kwa kosa lolote chini ya Sheria hii na maafisa polisi wote waliohukumiwa kwa kuzuiwa kinidhamu, wanaweza kufungiwa katika jengo lolote lililowekwa kwa ajili ya chumba cha ulinzi au chumba kidogo (seli) kwa ajili hiyo. [kifungu cha 60]
Namna ya malalamiko ya afisa polisi Gzt.Na. 73 la 1965
64. (1) iwapo inspekta yeyote, afisa isiyekuwa na kamisheni au konstabo anaona mwenyewe amekosewa katika jambo lolote tofauti na shtaka linalotuhumiwa chini ya Sehemu ya SABA na afisa polisi yeyote wa daraja la chini kuliko afisa msimamizi wa polisi katika kituo alichopangiwa, anaweza kulalamika kwa afisa msimamizi wa polisi, na kama anaona mwenyewe kuwa amekosewa na afisa polisi huyo msimamizi au afisa yeyote wa daraja sawa au la juu, na sio Kamishna, kutokana na malalamiko yake kutokufidiwa au kutokana na jambo lingine lolote tofauti na shtaka lolote chini ya Sehemu ya SABA, anaweza kulalamika kwa Waziri; na afisa polisi msimamizi, Kamishna au Waziri, kama itakavyoweza kuwa, kulingana na lalamiko lolote lililotengenezwa, atasababisha lalamiko hilo kufanyiwa uchunguzi, na kama kwenye uchunguzi ameridhika haki imetendeka, kuchukuwa hatua kama itakavyoweza kuwa lazima kwa kutoa fidia kwa lalamiko kutokana na jambo lililolalamikiwa kama inavyohitaji.
(2) Kila lalamiko hilo litatengenezwa katika namna iliyoelezwa na kanuni au amri zilizotengenezwa chini ya Sheria hii. [kifungu cha 61]
Kukatazwa dhidi ya afisa polisi kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi
65. (1) Haitakuwa halali kisheria kwa afisa polisi yeyote kuwa au kuja kuwa mwanachama wa:-
(a) chama chochote cha wafanyakazi, bodi yoyote au kuwa katika jumuiya iliyoshirikishwa katika chama cha wafanyakazi au;
(b) kundi lolote au jumuiya ambayo dhumuni lake ni kutawala na kulazimisha kulipa malipo ya uzeeni masharti ya utumishi wa Jeshi tofauti na kundi au jumuiya yoyote ambayo inaweza kuundwa na kudhibitiwa kulingana na kanuni zilizotengenezwa chini ya Sheria hii.
(2) Afisa polisi yeyote ambaye anakiuka masharti ya kifungu hiki atakuwa hatiani kwa kufukuzwa kutoka katika Jeshi na kupoteza haki zake zote zitokanazo na malipo ya uzeeni na kiinua mgongo.
(3) Kama swali lolote limejitokeza kwamba kikundi chochote ni chama cha wafanyakazi au ni jumuiya ambapo kifungu hiki kinatumika, swali hilo litaamuliwa na Mwanachama ambaye uamuzi wake utakuwa wa mwisho na hitimisho. [kifungu cha 62]
38
SEHEMU YA NANE
MFUKO WA TUZO WA POLISI
(kifungu cha 66)
Kuanzishwa kwa Mfuko wa Tuzo wa Polisi Gzt..Na. 478 la 1962; 73 la 1965
66. (1) Kwa kuongeza fedha ambapo chini ya aya ya (a) ya kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 47 au masharti yoyote ya Sheria hii au Sheria nyingine yoyote zimeelekezwa malipo yatalipwa kwa Inspekta Jenerali Mkuu, na yatawekwa katika mfuko utakaoitwa Mfuko wa Tuzo wa Polisi, fedha zifuatazo:-
(a) fedha zote zilizopo kwenye Mfuko wa Tuzo wa Polisi na Mfuko wa Faini Chini ya Sheria ya Polisi * imefutwa na Sheria hii;
(b) Faini zote zilizotolewa chini ya masharti ya Sheria hii au kanuni
zilizotengenezwa kwa mujibu wa Sheria hii kwa kosa lolote dhidi ya nidhamu;
(c) tuzo zote, fidia na faini ambazo kisheria zinalipwa kwa mtoa habari yeyote,
kama mtoa habari huyo ni afisa polisi; na
(d) fedha zote ambazo chini ya aya ya (b) ya kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 47 yameelekezwa kulipwa kwa mtafutaji wa mali zisizodaiwa, kamamtafutaji huyo ni afisa polisi.
(2) Katika kuongeza kiasi cha fedha kwenye Mfuko wa Tuzo wa Polisi chini ya kifungu kidogo (1) cha kifungu hiki Katibu Mkuu wa Hazina anaweza kuamuru kulipwa kwenye Mfuko huo kati ya mapato ya Jamhuri ya Muungano kiasi hicho cha fedha kama atakavyoona inafaa kinachotokana na vyanzo vifuatavyo:-
(a) Fedha zinazotokana na mapato ya Jamhuri ya Muungano kutokana na faini zinazotozwa katika mahakama yoyote kwa shambulio dhidi ya afisa polisi chini ya Sura ya XXV ya Sheria ya Makosa ya Jinai *;
(b) fedha au mabaki ya mali yoyote iliyotwaliwa kwenye mapato ya Jamhuri ya Muungano kwa amri ya mahakama kutokana na kosa lolote chini ya kifungu cha 91, 92 au 93 ya Sheria ya Makosa ya Jinai ambapo afisa polisi kama mtumishi wa umma anahusika;
(c) fedha zilipatikana na kulipwa katika mapato ya jumla ya Jamhuri ya Muungano chini ya kifungu cha 80 cha Sheria hii.
(3) Hakuna malipo yatakayotolewa kutoka katika Mfuko wa Tuzo wa Polisi isipokuwa kwa mamlaka ya Mrakibu Mkuu.
(4) Mrakibu Mkuu anaweza, kwa hiyari yake mwenyewe, kuidhinisha malipo kutoka kwenye Mfuko wa Tuzo wa Polisi kutokana na madhumuni yafuatayo:-
(a) msaada kwa wake au familia ya marehemu ambaye ni mwanachama wa Jeshi wa daraja la mrakibu au chini yake au kwa mwanachama yeyote aliyeondolewa katika Jeshi kwa kutokuwa na afya nzuri kwa huduma zaidi;
39
(b) mchango kwa ajili ya tuzo/zawadi zitakazotolewa katika mikutano ya riadha, shambulio la silaha na matukio mengine yanayoandaliwa na Jesh au kwa manufaa ya Jeshi;
(c) malipo kwa wanachama wa Jeshi wa daraja la mrakibu au chini kama tuzo ya kutunuku vitendo au utumishi katika kutekeleza majukumu, kama malipo hayo hayajalipwa kutoka mifuko ya kikoloni;
(d) matumizi kwa manufaa na maendeleo ya burudani na michezo iliyoidhinishwa na shughuli nyingine za polisi zilizoandaliwa ndani ya Jeshi. [kifungu cha 63]
SEHEMU YA TISA
VIINUA MGONGO NA RUZUKU AMBAZO ZINAWEZA KUTOLEWA KWA WANACHAMA FULANI WA JESHI TOFAUTI NA MAAFISA WANAOSTAHILI MALIPO YA UZEENI.
(kifungu cha 67-73)
Utumiaji wa vifungu vya 68 hadi 72. Sheria Na. 35 ya 1965kif. 3
67. Masharti ya kifungu cha 68 hadi 72 ya Sheria hii (tofauti na masharti yaliyopo katika aya (d) ya kifungu cha 69) yatatumika kwa maafisa wasiostahili pensheni wa daraja la chini ya Mrakibu Msaidizi tu na masharti ya aya (d) ya kifungu cha 69 yatatumika tu kwa maafisa wasiostahili pensheni wa daraja la chini ya sajini wa kituo tu. [kifungu cha 64]
Viinua mgongo vinavyolipwa baada ya miezi kumi na mbili au zaidi ya utumishi zaidi Sheria. Na. 1 ya 1958 kifungu cha 16; Gzt. Na. 73 la 1965
68. Kila afisa wa Jeshi ambaye kifungu hiki kinatumika, baada ya kuondolewa na kuongezewa muda wa utumishi kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili atastahili kupata kiinua mgongo kwa kiwango cha robo tatu ya mshahara wa mwezi kwa cheo au ofisi aliyokuwa anafanya kazi katika tarehe aliyoondolewa kwa mwaka mzima kwa kipindi kisichozidi miaka ishirini na moja:
Ilimradi kwamba kila afisa tofauti na afisa anayestahili pensheni ambaye ameorodheshwa katika Jeshi kabla ya tarehe 1 Januari, 1936, anaweza, wakati wa kuondolewa badala ya kupata kiinua mgongo kilichoelezwa hapa, kuchagua kupata kiinua mgongo hicho cha utumishi na msamaha wa kutokulipa kodi ya nyumba au kodi ya kichwa au pensheni au kiinua mgongo cha ziada kama ambavyo angekuwa anastahili kupata kwa mujibu wa masharti ya sheria inayotumika kabla ya tarehe 29 Oktoba, 1937. [kifungu cha 65]
Viinua mgongo vyenye uwiano kulipwa katika mazingira fulani. Sheria Na. 35 ya 1965 kifungu cha 3; Gzt.Na. 73 la 1965
69. Pale ambapo mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye kifungu hiki kinatumika:-
(a) amefariki;
(b) ameondolewa kutokana na kwamba kiafya hawezi kutumikia zaidi (kutokuweza huko kusiwe kumesababishwa na mwenendo wake mbaya au uzembe);
(c) ameondolewa kwa kupunguzwa; au
(d) kutokana na kuorodheshwa katika Jeshi kabla ya tarehe 8 Desemba, 1961, anatakiwa kustaafu au kuacha kutumikia Jeshi
40
kulingana na masharti ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Kustaafu ya Utumishi wa Umma, kabla ya kumaliza miaka kumi na mbili ya mwendelezo wa utumishi mzuri, Katibu Mkuu wa Hazina anaweza, kufuatia mapendekezo ya Inspekta Jenerali Mkuu, kuidhinisha malipo kwa wakala wake au mwenyewe, kama itakavyoweza kuwa, sehemu ya kiinua mgongo ambacho angeweza kuwa amekipata chini ya kifungu cha 68 kama angalikuwa amemaliza muda huo wa utumishi.
[kifungu cha 66]
Viinua mgongo vilivyopatikana kuchukuliwa kuwa kama sehemu ya mali ya afisa. Ord. No. 1 ya 1958; G.N. No. 73 ya 1965
70. Viinua mgongo vyovyote ambavyo vingeweza kulipwa kwa mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye kifungu hiki kinatumika, kama ameondolewa kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii, kama imetokea kuongezewa muda wa utumishi, vitachukuliwa kuwa vyake kwa madhumuni ya kugawanya mali zake. [kifungu cha 67]
Viinua mgongo visivyolipwa mpaka kifo: mpangilio ukoje. Ord. No. 1 ya 1958; G.N. No. 73 ya 1965
71. Pale ambapo mwanachama wa Jeshi ambaye kifungu hiki kinatumika kutokana na kuondolewa, amefariki kabla ya kupata kiinuua mgongo chochote ambacho anastahili kwa mujibu wa kifungu cha 68 au 69, kiinua mgongo hicho kitalipwa kwa mtu aliyeidhinishwa kugawa mali zake kama sehemu ya mali hiyo. [kifungu cha 68]
Fidia panapotokea kifo, dhara au uharibifu unaotokea wakati wa zamu/ kazi. Ord. Na. 1 ya 1958 kifungu cha 20; G.N. No. 73 ya 1965
72. Wakati wa kutekeleza majukumu yake, afisa yeyote wa jeshi ambaye kifungu hiki kinatumika, ameuawa au amejeruhiwa mpaka kusababisha kuondolewa kwake kutoka katika Jeshi, au mali zake zimeharibiwa wakati kutekeleza majukumu yake, Waziri, kwa mapendekezo ya Kamishna, anaweza kuelekeza malipo kutoka katika mapato ya umma kama fidia kama anavyoona inafaa; na fidia hiyo itakuwa ni nyongeza katika kiinua mgongo chochote ambacho anaweza kuwa anastahili kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii.
[kifungu cha 69]
Kiinua mgongo kwa waliopata tuzo.G.N. No. 73 ya 1965
73. Kila afisa wa Jeshi wa daraja la Meja Sajini au chini mwenye Medali ya Polisi ya Kiafrika au Medali ya Polisi ya Kifalme kwa Ushujaa au Utumishi uliotukuka au Medali ya Polisi ya Kikoloni kwa Ushujaa au Tunuku ya Utumishi aliyopata kutokana na utumishi katika Jeshi la Polisi la Tanganyika na Zanzibar, au medali yoyote au tuzo iliyotolewa na Rais kutokana na dhamani, ujasiri au ushujaa wakati wa utumishi katika Jeshi anaweza, kwa mapendekezo ya Kamishna na idhini ya Waziri bila kujali muda wa utumishi wake, kulipwa kiinua mgongo kama itakavyoamuliwa na Waziri.
[kifungu cha 70]
SEHEMU YA KUMI
MPANGILIO WA MALI ZA MAREHEMU
Masharti ya
74. (1) Inspekta Generali Mkuu ataweka au atahakikisha kuwekwa kwa
41
mpangilio wa mali ya maafisa waliofariki bila wosia G.N. No. 73 ya 1965
kumbukumbu binafsi za kila mwanachama wa Jeshi wa daraja la mrakibu au daraja la chini.
(2) Ikitokea afisa huyo wa Jeshi amefariki bila wosia wakati akiwa Jeshini taarifa ya kifo pamoja na kumbukumbu binafsi vitapelekwa kwa afisa mtawala mwandamizi wa wilaya aliyokuwa amepangiwa afisa huyo wakati wa kifo chake.
(3) Afisa polisi yeyote au afisa wa serikali ambaye anasimamia au kudhibiti malipo yoyote, kiinua mgongo, posho au fedha nyingine au mali binafsi za afisa yeyote yule wa Jeshi aliyetajwa katika kifungu kidogo cha (1) ambaye amefariki wakati anatumikia Jeshi, atalipa au atapeleka mali hizo kwa afisa utawala mwandamizi wa wilaya ambayo alipangiwa wakati wa kifo chake na atapanga mgawanyo wa mali hiyo kwa mujibu wa sheria.
[kifungu cha 71]
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
AJIRA YA MAAFISA POLISI KWA KAZI MAALUMU NA KUDUMISHA AMANI SEHEMU ZENYE GHASIA
(kifungu cha 75-80)
Ajira ya maafisa polisi kwa kazi maalum kwa gharama za watu binafsi
75. (1) Inspekta Jenerali Mkuu anaweza, kutokana na maelekezo ya Waziri, katika maombi ya mtu yeyote na baada ya kuridhika kutokana na umuhimu wa ombi hilo, kutoa namba yoyote ya maafisa polisi kwa ajili ya kazi maalum katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi ambacho kinaweza kuzingatiwa kuwa ni lazima. Maafisa polisi hao, kulingana na masharti ya Sheria hii, watakuwa chini ya amri ya afisa mwandamizi wa polisi katika sehemu hiyo na, isipokukuwa Waziri ameelekeza vinginevyo, wataajiriwa kwa gharama za mtu aliyefanya maombi:
Ilimradi kwamba mtu yeyote ambaye kwa maombi yake, maafisa polisi wametolewa kwa kazi maalumu katika sehemu yoyote anaweza kuomba maafisa polisi hao kuondolewa na ikimalizika mwezi mmoja kuanzia tarehe ya taarifa hiyo au kipindi kifupi zaidi kama Inspekta Jenerali Mkuu atakavyoona, mtu huyo atapunguziwa gharama nyingine zozote kulingana na ajira ya maafisa polisi hao.
(2) Kiasi chochote kitakachopatikana kama gharama kutoka kwa mtu yeyote aliyefanya maombi hayo chini ya kifungu kidogo cha (1) kinaweza kulipwa na Mrakibu Mkuu kama deni, na kitakapopokelewa kitalipwa kwenye mapato ya Jamhuri ya Muungano. [kifungu cha 72]
Ajira ya kuongeza ya polisi katika mazingira maalumu.
76. Pale ambapo Inspekta Jenerali Mkuu anaona kwamba ni kwa manufaa ya mtu yeyote kwamba ajira ya polisi katika sehemu yoyote ni lazima kwa usalama wa mali ya umma au binafsi, au kwamba kuna sababu za kuamini kuvunjika kwa amani, anaweza, kutokana ma maelekezo ya Waziri, kuwapanga maafisa polisi kikazi katika sehemu yoyote kwa kipindi hicho kama atakavyoona ni lazima, na anaweza kumuagiza mtu yeyote kulipa gharama zote au sehemu ya gharama zilizotumika, na mtu huyo baadaye atahakikisha malipo yamelipwa katika namna ambayo Inspekta Jenerali Mkuu
42
anaweza kuelekeza:
Ilimradi kwamba mtu yeyote ambaye amehitajika kulipa gharama hizo kama ilivyosema hapo juu anaweza kukata rufaa dhidi ya maagizo hayo kwa Waziri ambaye uamuzi wake utakuwa wa mwisho. [kifungu cha 73]
Ajira ya nyongeza ya polisi katika sehemu zenye ghasia
Sura ya kwanza
77. (1) Waziri anaweza, kwa amri kuitangaza, sehemu yoyote katika Jamhuri ya Muungano, kwamba sehemu hiyo ni sehemu ya ghasia na pia katika amri hiyo au inayofuata kiasi kwamba kuna hali isiyo ya kawaida na anaweza kutangaza tena kwamba anaweza kwa sababu ya vitendo vya wakazi wa eneo hilo, au tabaka lolote au sehemu ya wakazi hao, ni muhimu kuongeza idadi ya maafisa polisi waliopangwa katika sehemu hiyo.
(2) Baada ya kutangaza amri hiyo chini ya kifungu kidogo cha (1) Inspekta Jenerali Mkuu, kutokana na maelekezo ya Waziri, ataajiri idadi hiyo ya maafisa polisi kama nyongeza ya hao waliopangwa katika kituo kilichoainishwa katika amri hiyo kama atakavyoona inafaa, na, kutokana na masharti ya kifungu kidogo cha (3), gharama za hao maafisa polisi walioongezwa zitatolewa na wakazi wa eneo hilo.
(3) Pale ambapo maafisa polisi wa ziada wamepangiwa katika sehemu chini ya masharti ya kifungu kidogo (2) cha kifungu hiki, Mkuu wa Mkoa wa mkoa ambao sehemu hiyo ipo, baada ya uchunguzi kama atakavyoona inafaa na kutokana na maelekezo ya Waziri, kugawa gharama ya polisi hao wa ziada kati ya wakazi wa eneo hilo, na mgawanyo huo utafanyika kulingana na uchambuzi wa Mkuu wa Mkoa kulingana na uwezo wa wakazi hao:
Alimradi kwamba Mkuu wa Mkoa anaweza, kufuatia maelekezo ya Waziri, kumsamehe mtu yeyote au watu au kundi lolote au sehemu ya wakazi hao kutokulipa sehemu yoyote ya gharama hiyo.
(4) Amri yoyote iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) itaeleza kipindi ambacho itakuwa halali, lakini amri hiyo inaweza kwa wakati wowote kuondolewa au inaweza kuongezewa muda mara kwa mara kwa kipindi zaidi au vipindi kama Waziri atakavyoweza kuelekeza kwa kila kesi.
(5) Bila Kujali masharti ya Sheria ya Ufafanuzi, amri yoyote iliyotolewa chini ya kifungu hiki inaweza kutangazwa katika namna ambayo Waziri ataona inafaa. [kifungu cha 74]
[kifungu cha 74]
[ kifungu cha78]
78. (1) eneo lolote ambalo amri yoyote chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu cha 77 inatumika, kifo au maumivu au kupoteza au kuharibika kwa mali kumesababishwa au imetokana na vitendo vibaya vya wakazi wa eneo hilo au kundi lolote au sehemu ya wakazi hao, mtu yeyote ambaye amelalamika kupata hasara, uharibifu au kuumizwa kwa sababu ya vitendo hivyo vibaya anaweza, ndani ya mwezi mmoja baada ya tarehe ya hasara, uharibifu au kuumizwa kufanya maombi kwa ajili ya fidia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mkoa ambao sehemu hiyo ipo:
ila tu Mkuu wa Mkoa anaweza, kwa hiari yake mwenyewe mara kwa mara, kwa amri, kuongeza muda ambao maombi hayo ya fidia yanaweza kufanywa, lakini kiasi kwamba nyongeza hiyo kwa ujumla wake haitazidi miezi mitatu.
43
(2) Kufuatia madai hayo kufanyika, Mkuu wa Mkoa anaweza, kwa amri kutokana na maelekezo ya Waziri na baada ya uchunguzi kama atakavyoona inafaa, na labda ongezeko lolote la polisi limeshapangwa au halijapangwa katika sehemu hiyo chini ya kifungu cha 77:-
(a) kuamua mtu au watu ambao hasara, uharibifu au maumivu yamesababishwa au yametokana na vitendo vibaya;
(b) kuhakiki kiwango cha fidia kitakacholipwa kwa mtu huyo au watu na namna na uwiano ambao utakaogawanywa;
(c) kuhakiki uwiano ambao fidia italipwa na wakazi wa eneo hilo; na
(d) kuamuru malipo ya fidia hiyo:
Alimradi kwamba Mkuu wa Mkoa hatatoa amri yoyote chini ya kifungu hiki kidogo isipokuwa kama anaona kwamba hasara hiyo, uharibifu au maumivu yametokana na ghasia au mkutano usiokuwa halali ndani ya eneo hilo na kwamba mtu ambaye amepata hasara, uharibifu au maumivu hakuwa kwenye shutumu zilizotokana na matukio yaliyopelekea kwa hasara hiyo , uharibifu na maumivu:
Pia Mkuu wa Mkoa anaweza, kufuatia maelekezo ya Waziri, kwa amri yoyote kama ilivyotajwa hapo juu, au amri yoyote iliyofuatia, kumwondoa mtu yeyote au watu au tabaka lolote au sehemu ya wakazi hao katika wajibu wa kulipa sehemu yoyote ya fidia hiyo.
(3) Amri yoyote iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (2) itapitiwa na Waziri, lakini ukiacha kama ilivyosemwa hapo juu, itakuwa ya mwisho.
(4) Amri yoyote iliyotolewa kwa mujibu wa masharti ya kifungu hiki inaweza kuwasilishwa kwa mtu yeyote anayeathirika na amri hiyo katika namna ambayo Mkuu wa Mkoa atakavyoona inafaa.
(5) Kesi ya madai haitasikilizwa kufuatia hasara yoyote, uharibifu au maumivu ikiwa fidia imeshakubaliwa chini ya kifungu hiki. [kifungu cha 75]
Maana ya "wakazi"
79. Kwa madhumuni ya vifungu vya 77 na 78 neno "wakazi" inajumuisha watu wote ambao wao wenyewe au wakala wao au watumishi wao wanamiliki au wana maslahi halali katika ardhi au katika mali nyingine isiyohamishika ndani ya eneo lililoainishwa katika amri yoyote iliyotolewa chini ya kifungu cha 81 na wamiliki ardhi wote ambao wao wenyewe au wakala wao au watumishi hukusanya kodi moja kwa moja kutoka kwa wapangaji au wamiliki katika eneo hilo, bila kujali kwamba hawakai katika eneo hilo. [ kifungu 76]
Kupatikana na mpangilio wa pesa zilizolipwa chini ya sehemu ya KUMI NA MOJA
80. (1) Fedha zote zinazolipwa chini ya Sehemu hii ya Sheria hii zitapatikana katika namna iliyotolewa na sheria ya upatikanaji wa faini zitolewazo katika mashitaka ya jinai, au shitaka katika mahakama yoyote yenye mamlaka.
(2) Fedha zote zinazopatikana chini ya kifungu cha 75, 76 na 77 zitalipwa kwenye mapato ya jumla ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Fedha zote zinazopatikana chini ya kifungu 78 zitalipwa na Mkuu wa Mkoa kwa watu ambao wamelipwa kwa uwiano sawa. [kifungu 77]
44
SEHEMU YA XII
MAAFISA POLISI MAALUMU
Mamlaka ya kuteua maafisa polisi maalum kanuni na 22 ya 1955 kifungu cha 11; G.N. No. 73 ya 1965
81. (1) Pale ambapo inaonekana kwake kuwa ni kwa manufaa na usalama wa umma kufanya hivyo itakuwa ni halali kwa Inspekta Jenerali Mkuu au Inspekta msimamizi wa polisi, au Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya mwenye mamlaka katika mkoa au wilaya, kuteua kwa maandishi na mkono wake katika Fomu 2 ya Jedwali la Kwanza la Sheria hii wakazi wowote wa Jamhuri ya Muungano kuwa maafisa polisi maalum kwa idadi ambayo, kipindi ambacho, na ndani ya eneo hilo kama atakavyoona ni lazima.
(2) Endapo maafisa polisi wameteuliwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu hiki, Inspekta Jenerali Mkuu au afisa mwingine anayefanya uteuzi atapeleka kwa Waziri notisi ya uteuzi huo na mazingira ambayo yamepelekea uteuzi huo kuwa na manufaa. [kifungu 78]
Mamlaka ya kusimamishwa kwa muda na kubainisha utumishi wa maafisa polisi maalumu kanuni na. 22 ya 1955 kifungu cha 11
82. Inspekta Jenerali Mkuu au afisa mwingine ambaye ameteua afisa polisi maalum chini ya kifungu cha 81, anaweza kusimamisha kwa muda au kubainisha uteuzi wa afisa polisi maalumu yeyote kama ataona maanani kuwa uteuzi huo unaweza kusimamishwa kwa muda au kubainishwa na atapeleka taarifa kupitia fomu 3 ya Jedwali la Kwanza la Sheria hii kwa afisa polisi maalum anayehusika. [kifungu 79]
Rais anaweza kuanzisha Jeshi la maafisa polisi maalum C.A. Sheria No. 2 ya 1962
83. Bila kujali masharti ya kifungu 81 Rais anaweza, kama anaona inafaa, kuanzisha jeshi la maafisa polisi maalum na kuteua watu wa kuliongoza na anaweza kumuamuru Inspekta Jenerali Mkuu kuchagua katika jeshi watu wowote ambao wanaweza kutumikia na ambao anakubali utumishi wao na anaweza kutoa vyeo kwa maafisa polisi maalum hao na kutoa muda wa uteuzi wao au utumishi kulingana na masharti yanayofuatia hapa chini au kama itakavyoweza kuamriwa. [kifungu 80]
Maana ya "afisa polisi maalum" G.N. No. 73 ya 1965
84. Ukiacha pale ambapo maana inahitaji vinginevyo, katika sehemu hii ya Sheria “afisa polisi maalum" anajumuisha afisa yeyote ama ameteukiwa chini ya kifungu cha 81 au amechaguliwa chini ya kifungu cha 83. [kifungu 81]
Kukataa kwa mtu aliyeteuliwa kutumikia G.N. No. 73 ya 1965
85. (1) Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kwa maandishi au kwa namna nyingine kama atakavyoona inafaa kumuita afisa polisi maalum kutekeleza majukumu au mafunzo kama atakavyoona inafaa.
(2) Kama afisa polisi maalum, baada ya kuitwa kutekeleza majukumu au mafunzo kwa mujibu wa masharti ya kifungu hiki, amekataa au amezembea kutumikia, kwa kila katalio au uzembe atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kutoa faini isiyozidi shilingi mia moja , labda airidhishe mahakama kuwa alikuwa amezuiwa na ugonjwa au sababu nyingine zisizozuilika kama itakavyoweza kuwa kwa maoni ya mahakama ni sababu ya kutosha. [kifungu 82]
45
Mamlaka na Wajibu wa maafisa polisi maalum GN. No. 73 ya 1965
86. Kila afisa polisi maalum:-
(a) anapoitwa kutekeleza wajibu au mafunzo chini ya kifungu 85 cha Sheria hii; au
(b) Kama ameamriwa na afisa polisi yeyote ambaye sio wa daraja la chini ya inspekta kumsaidia polisi katika kutekeleza wajibu wao, atakuwa na mamlaka sawa, marupurupu na kinga kama afisa polisi wa daraja hilo na atawajibika kutekeleza wajibu sawa na atakuwa na haki ya fidia sawa na atakuwa chini ya mamlaka husika kama afisa polisi. [kifungu cha 83]
Inspekta Jenerali Mkuu kuwapatia maafisa polisi maalumu vifaa muhimu.
87. Itakuwa ni halali kwa Inspekta Jenerali Mkuu kuwapatia kwa gharama ya Serikali matumizi ya maafisa polisi maalum sare, beji, vifaa, silaa na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya kutekeleza vizuri majukumu ya ofisi yao.
[kifungu cha 84]
Sare, n.k, kurudishwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha uteuzi G.N. No. 73 ya 1965
88. Kila afisa polisi maalum, ndani ya wiki moja baada ya kukamilika kwa uteuzi wake au utumishi, atapeleka katika mpangilio mzuri (uchakavu wa mapungufu ya kawaida unatarajiwa) katika kituo cha polisi kilichopo karibu, fomu yake ya uteuzi au nyaraka za utumishi na sare yoyote, beji, kifaa, silaha au vifaa vingine ambavyo anaweza kupewa chini ya Sheria. Afisa polisi maalum yeyote ambaye anakataa au anazembea kupeleka atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kutoa faini isiyozidi elfu arobaini na mahakama inaweza kutoa hati ya kupekuwa na kukamata fomu zozote za uteuzi, nyaraka, sare, beji, vifaa, silaa au vyombo vingine ambavyo vitakuwa havijapelekwa. [kifungu 85]
Inspekta Jenerali Mkuu kusimamia G.N. No. 73 ya 1965
89. Inspekta Jenerali Mkuu, kufuatia maelekezo ya jumla ya Waziri, atakuwa na mamlaka, usimamizi na maelekezo ya afisa polisi maalum, na kufuatia masharti ya Sheria hii na kwa kanuni zozote zilizotengenezwa chini ya Sheria hii, anaweza kufanya uteuzi huo, kupandisha na kupunguza vyeo kama atakavyoona inafaa. [kifungu 86]
Kulipwa pale panapotokea kifo, dhara, uharibifu wa mali wakati wa kazi G.N. No. 73 ya 1965
90. (1) Kama afisa polisi yeyote maalum amepata kilema cha maisha au cha muda, kilichotokana na jeraha lolote au dhara au ugonjwa aliyoambukizwa wakati anatekeleza majukumu yake au mafunzo katika mazingira yaliyotajwa katika aya ya (a) na (b) ya kifungu cha 86 cha Sheria hii, au kama mali ya afisa polisi maalum yeyote imeharibiwa wakati wa kutekeleza majukumu hayo au mafunzo, Waziri anaweza kumlipa afisa polisi maalumu huyo fidia hiyo, kiinua mgongo au pensheni kama atakavyoona ni haki.
(2) Kama afisa polisi maalum yeyote ameuawa au amefariki kutokana na jeraha lolote au dhara alilolipata au ugonjwa alioambukizwa katika mazingira yaliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1), Waziri anaweza kutoa kwa wategemezi wa afisa polisi huyo maalum pensheni hiyo au malipo kama atakavyoona ni haki.
(3) Hakuna pensheni, fidia, malipo au kiinua mgongo kinacholipwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu hiki kitakaimishwa, kuhamishwa au
46
kuzuiwa au kukatwa kodi kwa utaratibu wowote wa kisheria. [s. 87]
SEHEMU YA XIII
UTUMISHI NJE YA JAMHURI YA MUUNGANO
(kifungu cha 91-98)
Waziri anaweza kutuma maafisa polisi katika nchi za jirani G.N. No. 73 ya 1965 Jedwali la Pili.
91. (1) Waziri anaweza, kutokana na maombi ya Serikali ya nchi yoyote ya jirani, kama ameridhika kwamba mpango wa makubaliano umefanyika au utafanyika na serikali hiyo kwa manufaa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kuamuru idadi hiyo ya maafisa polisi kama atakavyoona inafaa kwenda kutumika katika nchi hiyo nyingine.
(2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki na Sehemu hii ya Sheria hii “nchi jirani” maana yake ni nchi yoyote ambayo imepakana na Jamhuri ya Muungano na nchi nyingine yoyote kama Waziri atatangaza kupitia notisi itakayotolewa kwenye Gazeti la Serikali, kutangaza kuwa ni nchi ya jirani kwa madhumuni ya Sehemu hii ya Sheria hii. [kifungu. 88]
Kupeleka maafisa polisi katika nchi za jirani wakati wa dharura ya muda kanuni Na. 1 ya 1958 kifungu. 21; G.N. No. 73 ya1965 jedwali la pili.
92. (1) Endapo imetokea dharura ya muda Inspekta Jenerali Mkuu, au Kamishna msaidizi, au mrakibu msaidizi wa polisi katika jimbo lolote, ambaye ana mamlaka katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano ambayo imepakana na nchi yoyote ya jirani, anaweza, kutokana na maombi ya afisa tawala yeyote au afisa polisi yeyote mwenye kamisheni au aliyeandikwa katika Gazeti wa nchi hiyo, kuamuru maafisa polisi wowote ambao wako chini ya usimamizi wake, isiyozidi idadi iliyoombwa, kwenda kutumikia nchi hizo:
Ilimradi kwamba Kamishna Msaidizi yeyote msimamizi wa mkoa au mrakibu msimamizi yeyote wa polisi katika mkoa, ambaye hayuko chini ya amri za Kamishna Msaidizi, kila inavyowezekana, lazima apate kwanza idhini ya Mrakibu Mkuu kwa kitendo hicho kama ilivyotajwa hapo juu na kwa namna yoyote atatoa taarifa ya kitendo hicho kwa Kamishna haraka sana iwezekanavyo:-
(2) Maafisa polisi wote wa Jamhuri ya Muungano ambao wanaweza kuwa wameamriwa chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki kwenda kutumikia katika nchi ya jirani, watafuata amri hiyo, na kila amri itahesabiwa kuwa imetolewa na Waziri kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 91.
[kifungu cha 89]
Maafisa polisi wanaotumikia nje ya Jamhuri ya Muungano kuwa chini ya maafisa wao wenyewe na kufuatia sheria na amri zao wenyewe G.N. No. 73 ya 1965 Jedwali la Pili.
93. (1) Maafisa polisi wote wanaotumikia nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa masharti ya Sehemu hii watakuwa chini ya amri za maafisa wao waandamizi, kutegemea kufuatia usimamizi wa afisa mwandamizi aliyepo, awe ni afisa wa Jeshi au wa jeshi la polisi la nchi ya jirani na, kwa kadiri inanyohusiana na vigezo na masharti ya kazi na udumishaji wa nidhamu, atatawaliwa na vifungu nya sheria hii pamoja na kanuni zingine zozote zilizotungwa chini ya Sheria hii, na kadiri inavyowezekana, watatekeleza wajibu sawa kama walivyokuwa wanatumikia katika Jamhuri ya Muungano lakini kiasi kwamba, isipokuwa kama ilivyotajwa hapo juu, hakuna kitu katika Sehemu hii ya Sheria hii kitatumika kinyume na sheria ya jumla wakati ikiwa inatumika katika Jamhuri ya Muungano, ambayo itatumika na kuheshimiwa na
47
maafisa polisi katika namna sawa kama vile walikuwa maafisa polisi waliowekwa kutumikia katika nchi tajwa.
(2) Mamlaka yanayotolewa na Sheria hii kwa afisa yeyote, ambaye siyo Mrakibu Mkuu, kuadhibu makosa yanayotendwa na maafisa polisi yanaweza kutolewa na Mrakibu Mkuu kwa afisa yeyote wa Jeshi anayetumikia nchi hiyo.
[Kifungu 90]
Masharti tangulizi kutimizwa na sheria ya nchi husika
94. Maafisa polisi hawatapelekwa katika nchi jirani isipokuwa na mpaka pale Waziri atakaporidhika kwamba masharti ya kuridhisha yameshawekwa au yatawekwa kwenye sheria ya nchi husika:-
(a) kwa ajili ya kutumika, katika Serikali ya nchi kutolea huduma kati ya Maafisa Polisi wa Jeshi na Serikali ya nchi hiyo;
(b) kwa kuwapa maafisa polisi wa Jamhuri ya Muungano wanaotumikia katika nchi hiyo chini ya Sehemu hii mamlaka na wajibu wa maafisa polisi ndani ya nchi hiyo; na
(c) kwa kuiwezesha mahakama na mahakimu wa nchi hiyo wanaotumikia nchi hiyo kusikiliza na kuamua mashtaka dhidi ya maafisa polisi wa Jamhuri ya Muungano kutokana na makosa yaliyotajwa katika Sheria hii na kutoa adhabu, ambayo haitakuwa kubwa kuliko ilivyotajwa katika Sheria hii kutokana na makosa hayo. [kifungu. 91]
Maafisa polisi kutoka nchi za jirani kutumikia Jamhuri ya Muungano kuwa chini ya sheria zao, amri zao na maafisa wao wenyewe
95. Wakati wowote:-
(a) katika kujibu maombi yaliyofanywa na Waziri maafisa polisi yeyote wa jeshi la polisi la nchi ya jirani wapo katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano; au
(b) katika kujibu maombi yaliyoombwa na afisa yeyote wa utumishi wa umma wa Jamhuri ya Muungano maafisa polisi wowote kutoka nchi jirani wapo katika Jamhuri ya Muungano kwa madhumuni ya kusaidia Jeshi katika dharura yoyote ya muda,
Maafisa polisi hao watakuwa chini ya amri ya maafisa wao wenyewe waliokuwa nao kama wapo, kutategemea usimamizi wa afisa polisi mwandamizi aliyekuwepo, awe mwanachama wa Jeshi au wa jeshi la polisi la taifa la jirani, na, ikiwa haipingani na sheria nyingine zinazotumika na kama itakavyowezekana kutekeleza wajibu sawa kama walivyokuwa wanatumikia katika Jamhuri yao ya Muungano. [kifungu. 92]
Utekelezaji wa mkataba uliofanywa na Serikali ya nchi ya jirani.G.N. No. 73 ya 1965
96. Kila wakati ambapo afisa polisi kutoka nchi jirani yupo katika Jamhuri ya Muungano chini ya mazingira yaliyotajwa katika kifungu cha 95, mkataba wowote wa huduma uliofanywa kati ya afisa huyo na Serikali ya nchi hiyo ya jirani unaweza kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano katika namna sawa na kwa matokeo sawa kama vile mkataba huo umefanywa kati ya afisa polisi huyo na Jamhuri ya Muungano. [Kifungu 93]
Mamlaka ya wanachama wa jeshi la polisi la nchi ya jirani
97. Mwanachama yeyote wa jeshi la polisi la nchi ya jirani aliyekuwepo katika Jamhuri ya Muungano chini ya mazingira yaliyotajwa katika kifungu cha 95 atakuwa na uwezo wa kutumia mamlaka na atawajibika kutekeleza
48
wajibu wa afisa polisi wa Jamhuri ya Muungano. [kifungu 94]
Mamlaka ya Mahakama za Jamhuri ya Muungano G.N. No. 73 ya 1965
98. Mahakama Kuu au mahakama yoyote ya chini ya Jamhuri ya Muungano inaweza kusikiliza na kuamua mashtaka dhidi ya maafisa polisi wa taifa la jirani waliopo katika Jamhuri ya Muungano chini ya mazingira yaliyotajwa katika kifungu cha 95 katika namna sawa kama mahakama ya nchi hiyo. [kifungu 95]
SEHEMU YA XIV
MASHARTI YA JUMLA
Mamlaka ya kuendesha mashtaka chini ya sheria nyingine bila kuathirika.
99. Sheria hii haitamuondoa mtu yeyote katika kushtakiwa chini ya sheria nyingine kutokana na kosa lolote linaloadhibiwa na Sheria hii, au kwa kuwa na hatia chini ya sheria nyingine yoyote au adhabu kubwa kuliko ilivyowekwa na Sheria hii:
Ilimradi hakuna mtu atakayeadhibiwa mara mbili kwa kosa hilo hilo.
[kifungu. 96]
Uasi Sheria No. 19 of 1964 kifungu. 2; G.N. No. 73 ya 1965
Sura 126
100. (1) Mwanachama yeyote wa Jeshi ambaye:-
(a) Anashiriki katika uasi unaohusiana na utumiaji wa nguvu au kutishia kutumia nguvu; au
(b) Anashawishi askari yeyote wa Jeshi au askari yeyote wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania au Jeshi la Kujenga Taifa, au Askari Magereza kushiriki katika uasi wowote, iwe halisi au iliyodhamiriwa, anatenda kosa na endapo atapatikana na hatia mbele ya Baraza Maalum atahukumiwa adhabu ya kifo au kifungo cha maisha au kipindi chochote pungufu.
(2) Afisa yeyote wa Jeshi ambaye, katika kesi isiyoanguka kati ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, ameshiriki katika uasi au incites mtu yeyote kama ilivyotajwa katika aya ya (b) ya kifungu kidogo cha (1) kushiriki katika uasi, iwe halisi au iliyodhamiriwa, anatenda kosa na atahukumiwa na Baraza Maalum kifungo cha maisha au kipindi chochote pungufu.
(3) Katika kifungu hiki:-
“uasi” maana yake ni muungano wa wanajeshi au zaidi wa Majeshi au Utumishi uliotajwa katika aya ya (b) ya kifungu kidogo cha (1) au kati ya watu ambao angalau wawili kati yao ni wanajeshi au Utumishi:-
(a) kupindua au kukataa mamlaka halali ya Jeshi hilo au Utumishi; au
(b) Kutokutii mamlaka iliyopo katika mazingira ambayo yatafanya ukosefu wa nidhamu; na
'Baraza Maalum' maana yake ni baraza lililoanzishwa chini ya Sheria ya Mabaraza Maalum.* [kifungu 97]
Maafisa polisi walioondolewa kati ya tarehe fulani kutakiwa kutoa taarifa Sheria No.
101. Pale ambapo mtu yeyote ameondolewa katika Jeshi kati ya tarehe ishirini na nane Januari, 1964 na siku ya kwanza ya Aprili, 1964, wakati wa kuondolewa atatakiwa na afisa polisi yeyote mwandamizi kutoa taarifa, iwe kila kipindi au la, kwa mtu yeyote mwenye ofisi anayetumikia katika Jamhuri,
49
19 ya 1964 kifungu cha 2
mtu yeyote aliyetajwa mwanzo ambaye anashindwa, bila sababu ya kihalali au ya msingi, kutoa taarifa kulingana na masharti ya uhitaji huo, mpaka anaondolewa katika uhitaji huo na mtu ambaye anatakiwa kupewa taarifa, atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa na mahakama hakimu mkazi au mahakama ya wilaya, kifungo kisichozidi mwaka mmoja au faini isiyozidi shilingi elfu moja au vyote kwa pamoja kifungo na faini. [kifungu cha 98]
Kutelekeza
102. (1) Mwanajeshi ambaye ametelekeza Jeshi atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kwa kifungo cha miezi sita.
(2) Mtu yeyote asitiwe hatiani kwa kosa kwa kosa la kutelekeza isipokuwa mahakama imeridhika kwamba alidhamiria kutokurudi tena Jeshini.
Kumiliki vifaa alivyopewa afisa polisi kinyume.
103. (1) Mtu yeyote, ambaye sio afisa polisi:-
(a) amepatikana anamiliki kifaa chochote ambacho alikuwa amepewa afisa polisi kutumia katika kutumia katika kutekeleza wajibu wake; au
(b) amepatikana anamiliki medali yoyote au pambo alilotunukiwa afisa polisi yeyote kwa ushujaa utumishi au matendo mazuri,
na anashindwa kueleza kwa kuridhisha kuhusu umiliki huo atakuwa na hatia ya kosa.
(2) Mtu yeyote ambaye, bila mamlaka halali:-
(a) ananunua au anapata kifaa chochote ambacho alipewa afisa polisi kutumia katika kutekeleza wajibu wake au medali yoyote au pambo alilotunukiwa afisa polisi yeyote kwa ushujaa, utumishi au matendo mazuri; au
(b) atamsadia au kuhamasisha afisa polisi yeyote katika kuuza au kuhamisha kwa kifaa hicho, medali au pambo,
atakuwa na hatia ya kosa [kifungu 100]
Kulinda nyumba za umma za maafisa polisi wakati wakiwa kazini.
104. Mtunzaji yeyote wa nyumba, stoo au sehemu ambayo kinywaji kikali kinauzwa ambaye, yeye mwenyewe au na mtu yeyote aliyemwajiri, kwa kujua anamuhifadhi au anamuendekeza mwanachama yeyote wa Jeshi au anaruhusu mwanachama huyo wa Jeshi kuwa kama mteja au mgeni katika nyumba hiyo, stoo au sehemu, wakati ambao muda huo mwanachama huyo wa Jeshi alikuwa zamu, atakuwa na hatia ya kosa na atahukumiwa kwa faini isiyozidi shilingi mia nne au kifungo kisichozidi miezi mitatu. [kifungu 101]
Watu wanaosababisha chuki, n.k.
105. Mtu yeyote ambaye:-
(a) anasababisha au anajaribu kusababisha au anatenda kitendo kinachohesabika kusababisha chuki kati ya maafisa polisi;
(b) analazimisha au anajaribu kulazimisha au anafanya kitendo kinachohesabika kumlazimisha afisa polisi yeyote kupelekea kukosa nidhamu,
Atakuwa na hatia ya kosa na atahukumia kutoa faini isiyozidi shilingi elfu moja au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja faini na kifungo. [kifungu 102]
50
Vitendo visivyokubalika katika kituo cha polisi, ofisini na mahabusu
106. (1) Mtu yeyote ambaye, katika kituo cha polisi chochote au ofisi ya polisi au mahabusu, anafanya fujo, hajiheshimu, hatii amri au anatenda kosa.
(2) Afisa polisi yeyote anaweza kumkamata bila kibali mtu yeyote, kwa mawazo yake, anayetenda kosa lolote kwa mujibu wa masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki. [kifungu 103]
Adhabu ya jumla
107. Mtu yeyote ambaye anatenda kosa hatia ya kosa kwa mujibu wa masharti yoyote ya Sehemu ya KWANZA hadi KUMI NA NNE ambapo hakuna adhabu nyingine yoyote iliyotolewa, atahukumiwa kutoa faini isiyozidi shilingi mia tano, au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote kwa pamoja faini na kifungo. [kifungo. 104]
SEHEMU YA KUMI NA TANO
AKIBA YA POLISI
[9 Juni, 1939]
(kifungu 108-124) Ords. Nos. 1 ya 1939; 14 ya 1950; 27 ya 1954; 43 ya 1958
Kuanzishwa kwa Akiba ya Jeshi.
Muundo wa Akiba ya Jeshi. 43 s. 4
Usimamizi wa Akiba ya Polisi [Sheria Na. 43 ya 1958 kifungu cha 3]
Azimio kutolewa wakati wa uandikishwaji.
Kipindi cha utumishi katika Akiba.
Cheo kugawiwa kwa askari wa akiba
108. Inaweza kuanzishwa na kudumishwa Akiba ya Polisi.
[kifungu 105]
109. Iwapo Akiba ya Polisi imeanzishwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 108, itajumuisha afisa polisi wa akiba wenyeji walioorodheshwa au kuajiriwa upya kulingana na masharti ya Sheria hii. [kifungu 106]
110. Kama akiba ya polisi imeanzishwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 108, utawala na mamlaka ya akiba hiyo yatakuwa chini ya Mrakibu Mkuu.
[kifungu 107]
111. Kila mtu ambaye amekubali kuandikishwa katika Akiba ya Polisi ataweka azimio katika fomu iliyopo kwenye Jedwali la Tatu la Sheria hii mbele ya hakimu au afisa aliyetangazwa kwenye gazeti la serikali na mara tu baada ya kufanya azimio hilo atakuwa askari wa Akiba ya Polisi. [s. 108]
112. Kila askari wa akiba ataorodheshwa kwa kipindi kinachojulikana ambacho hakizidi miaka mitatu; na anaweza mara kwa mara kufuatia idhini ya Inspekta Jenerali Mkuu, kurudishwa kwa kipindi hicho hicho.
[kifungu cha 109]
113. Itakuwa ni halali kwa Inspekta Jenerali Mkuu kugawa kwa kila askari wa akiba cheo ambacho anaona askari huyo wa akiba kinamfaa.
51
Haki ya kujiondoa katika mazingira fulani
Malipo na posho. Sheria. Na. 14 ya 1950 kifungu. 2
Wajibu wa askari wa akiba.
Kuhitajika kwa Akiba ya Polisi kwa mafunzo ya mwaka. Sheria Na. 43 ya 1958 kifungu 6
Kutoa Akiba ya Polisi kwa ajili ya kutumikia panapotokea dharura.
Sheria Na.14 ya mwaka 1950 kifungu cha 3
[kifungu cha. 110]
114. Ikitokea kwamba askari wa akiba ambaye ametumikia Jeshi la Polisi la Tanzania amepewa cheo cha chini kuliko alichokuwa nacho wakati anaondolewa katika Jeshi ataruhusiwa kujiondoa kwenye Akiba iwapo kama anataka. [kifungu cha 111]
115. (1) Isipokuwa kama ilivyotajwa na kifungu kidogo cha (2) cha kifungu hiki kila askari wa akiba atalipwa mara nne kwa mwaka katika kiwango sawa cha mwezi kama itakavyoweza kuamuliwa na Waziri mara kwa mara na anaweza kupokea, kama nyongeza, posho nyingine kama Waziri atakavyoamua.
(2) Iwapo masharti ya kifungu cha 117 au 118 yatatumika kila askari wa akiba atapokea malipo na posho ya cheo chake. [kifungu 112]
116. Kila askari wa akiba:-
(a) ataripoti mwenyewe kwa vipindi tofauti kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu kwa afisa msimamizi wa polisi katika kituo kilicho karibu na mahali anapoishi au Afisa Wilaya;
(b) atamjulisha afisa polisi huyo msimamizi wa Polisi au Afisa Wilaya mabadiliko yoyote ya anwani;
(c) atapata ruhusa ya mrakibu msaidizi wa polisi kabla ya kuondoka Jamhuri ya Muungano;
(d) iwapo atahitajika kwa ajili ya mafunzo au utumishi chini ya masharti ya kifungu cha 117 au 118, atahudhuria katika muda na sehemu aliyojulishwa. [kifungu 113]
117. Ikiwa Akiba ya Polisi imeanzishwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 108 itahitajika na Mrakibu Mkuu wa Polisi kwa ajili ya mafunzo ya mwaka katika sehemu hizo na kwa vipindi visivyozidi siku arobaini na mbili katika mwaka wowote kama atakavyoona inafaa:
Ilimradi kwamba Waziri anaweza, kwa amri, kuelekeza kwamba mafunzo ya mwaka yote au sehemu ya Akiba ya Polisi yasifanyike au yafupishwe. [kifungu. 114]
118. (1) Ikitokea vita, maasi au dharura nyingine, Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi anaweza, kwa kibali cha Waziri kutoa Akiba ya Polisi au sehemu yoyote ya Akiba hiyo kutumikia Jeshi.
(2) Askari wa akiba ya polisi aliyetolewa kwa mujibu wa masharti ya kifungu hiki anaweza kuhitajika kuendelea na utumishi wake kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili zaidi ya kipindi chake cha kuorodheshwa wakati wa kuitwa. [kifungu cha 115]
119. Taarifa kutolewa kwa askari wa akiba wanapotakiwa kwa ajili ya mafunzo.
Askari wa akiba atapewa taarifa itakayotolewa na mamlaka ya Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi kuhudhuria mafunzo au utumishi, kama itakavyokuwa
52
Kuitwa kwa askari wa akiba chini ya masharti ya Sheria hii. Sheria Na. 43 ya 1958 kifungu cha 7
Adhabu. Sheria Na. 27 ya 1954 kifungu. 2; 43 ya 1958 kifungu. 8
Kuondolewa kwa askari wa akiba
Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kufuta utumishi wa askari wa akiba
Viinua Mgongo. Sheria Na. 27 ya 1954 kif. 3
kwa wakati na mahali palipotajwa; taarifa hiyo itatumwa au itawasilishwa katika sehemu ya mwisho inayojulikana kama makazi ya askari wa akiba huyo na itadhaniwa kuwa taarifa hiyo imemfikia, isipokuwa kama itaonekana vinginevyo. [kifungu cha 116]
120. Kila askari wa akiba, wakati wa kutolewa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 117 au kifungu cha 118, atakuwa anaheshimu masharti ya Sheria hii kiasi kwamba masharti hayo hayagongani au kukinzana na masharti ya Sheria hii. [kifungu cha 117]
121. (1) Ikitokea kwamba askari wa akiba anashindwa kufuata masharti yoyote ya aya ya (a), (b) au (c) ya kifungu cha 116, afisa polisi aliyeandikishwa katika gazeti anaweza, baada ya upelelezi, na kama askari wa akiba huyo ameshindwa kuonyesha sababu ya msingi ya kushindwa kufuata masharti hayo, atampa adhabu askari huyo wa akiba ya kutoa faini isiyozidi shilingi kumi, ambayo itatolewa katika mshahara wake.
(2) Askari wa akiba yeyote ambaye amepewa taarifa chini ya masharti ya kifungu cha 117 au kifungu cha 118 na ambaye, bila ya sababu ya msingi, anashindwa kuhudhuria kwa wakati na sehemu aliyojulishwa ana hatia ya kosa na anawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miezi sita.
(3) Askari wa akiba ambaye anauza, anaweka rahani, anaharibu au vinginevyo anajiweka mbali na medali yoyote au nishani nyingine aliyotunukiwa kutokana na utumishi wake ana hatia ya kosa na anawajibika kutoa faini ya shilingi kumi au, akishindwa kulipa, kifungo ch siku kumi na nne.
(4) Kwa madhumuni ya kifungu cha 26 cha Sheria hii askari wa akiba atahesabika kutokuwa sehemu ya Jeshi:-
(a) pale ambapo anaacha kuwa askari wa akiba; au
(b) pale ambapo kipindi chake alichotolewa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 117 au 118 kimemalizika. [kifungu 118]
122. Kila askari wa akiba ambaye amemaliza kipindi chake au vipindi vya utumishi na Akiba ya Jeshi kulingana na masharti ya Sheria hii na kila askari wa akiba ambaye utumishi wake umetolewa chini ya masharti ya kifungu cha 123 ataondolewa na atapewa cheti cha kuondolewa katika namna ambayo kama Mrakibu Mkuu atakavyoona inafaa. [kifungu cha 119]
123. Katika muda wowote pale ambapo askari hajaitwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 117 na 118 utumishi wa askari wa akiba unaweza kufutwa na Mrakibu Mkuu kwa kutoa notisi ya mwezi mmoja kwa maandishi:
Ikiwa, utumishi wa askari wa akiba umefutwa na Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi kufuatia maombi ya askari wa akiba mwenyewe, notisi hiyo haitakuwa ya lazima. [kifungu cha 120]
124. (1) Kila askari wa akiba ambaye kifungu hiki kinatumika wakati wa kuondolewa baada ya utumishi mzuri wa kipindi kisichozidi miaka kumi na mbili mfululizo, atastahili kupata kiinua mgongo kilichokokotolewa kwa
53
kiwango cha mbili ya tatu ya mshahara wa mwezi katika cheo ambacho anatumikia wakati wa tarehe ya kuondolewa kutoka katika Jeshi kwa kila mwaka wa utumishi uliomalizika kwa kipindi kisichozidi miaka kumi na mbili.
(2) Pale ambapo askari wa akiba ambaye kifungu hiki kinatumika anafariki au anaondolewa kutokana na kutokuwa na hali nzuri kiafya kuendelea kutumikia Akiba ya Jeshi (matatizo hayo ya kiafya yaliyosababishwa na mwenendo wake mbaya au uzembe wake) au kutokana na kupunguzwa kwa uanzishwaji, kabla ya kumaliza miaka kumi na mbili ya mfululizo wa utumishi mzuri, Waziri anaweza, kufuatia mapendekezo ya Inspekta Jenerali Mkuu kuidhinisha malipo kwa wakala wake au yeye mwenyewe, kama itakavyoweza kuwa, ya sehemu inayoendana na kiinua mgongo ambacho angeweza kupata chini ya kifungu kidogo cha (1) kama angekuwa amemaliza kipindi hicho cha utumishi.
(3) Kifungu hiki kitatumika kwa askari yeyote wa akiba ambaye ameondolewa katika Jeshi baada ya kumaliza kipindi chake au vipindi nyake vya utumishi kulingana na masharti ya Sheria hii, na ndani ya mwezi mmoja baada ya kuondolewa, au kipindi hicho kirefu kama Mrakibu Mkuu anavyoweza kuruhusu katika kesi yoyote mahsusi, kuandikishwa tena katika Akiba ya Polisi.
(4) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (1) na kifungu kidogo cha (2), "utumishi" maana yake ni utumishi katika Akiba ya Polisi pamoja na utumishi wowote na Jeshi kulingana na masharti ya Sheria hii.
[kifungu cha 121]
SEHEMU YA KUMI NA SITA
JESHI LA POLISI SAIDIZI
(vifungu 125-147)
[13 Augusti, 1948]
Sura ya 11
125. Katika Sehemu hii, isipokuwa itahitajika vinginenyo:-
"Jeshi la Polisi Saidizi" maana yake Jeshi la Polisi Saidizi lililoanzishwa chini ya masharti ya kifungu cha 126;
"afisa polisi saidizi " maana yake mwanachama yeyote wa Jeshi la Polisi Saidizi;
"afisa mwenye cheo" inajumuisha Mrakibu Msimamizi, inajumuisha Mrakibu, Inspekta Msimamizi Msaidizi na mwanafunzi katika shule ya maofisa wa Jeshi;
"hakimu" maana yake ni Hakimu aliyeteuliwa chini ya vifungu vya Sheria ya Mahakama ya Mahakimu *;
"afisa polisi mwandamizi" maana yake mwanachama wa Jeshi la Polisi Saidizi mwenye cheo kinachoendana na afisa mwenye cheo;
"eneo maalum" maana yake ni eneo la Tanzania lililotangazwa kuwa eneo maalum chini ya masharti ya kifungu cha 129;
"kazi ya kibali" maana yake ni kampuni , shirika au bodi ya kisheria.
[kifungu. 122]
54
Kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi Saidizi.
126. Kutaanzishwa Jeshi la Polisi ambalo litakuwa ziada katika Jeshi
[kifungu 12
Kazi za Jeshi la Polisi Saidizi.
127. Jeshi la Polisi Saidizi litasaidia Jeshi katika kudumisha amani na kulinda mali katika maeneo maalum. [kifungu. 124]
Mamlaka ya jumla ya Inspekta Jenerali Mkuu.
128. Inspekta Jenerali Mkuu, kutegemeana na maelekezo ya jumla ya Rais, atakuwa na amri na atasimamia Jeshi la Polisi Saidizi kama inavyostahili, na atawajibika kwa Rais kwa utekelezaji stahili wa vifungu vya Sheria hii.
[kifungu cha. 125]
Kutangazwa kwa maeneo maalum. Sheria Na. 19 ya 1969 kifungu cha 6
129. Iwapo Rais ameridhishwa kwamba sehemu iliyopewa kibali inajishughulisha na biashara, viwanda, kilimo, ufugaji, ujenzi, maendeleo ya madini ya Jamhuri ya Muungano au sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano au maendeleo yoyote mengine katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano, na hayo masharti maalum yanatumika kuimarisha sehemu ambayo maendeleo hayo yanapatikana, Rais anaweza, kufuatia maombi ya shughuli hiyo, kwa kutoa notisi katika gazeti la serikali, kutangaza kuwa eneo hilo au sehemu ya eneo hilo kuwa sehemu maalum kwa madhumuni ya Sheria hii. [kifungu cha 126]
Jeshi la Polisi Saidizi kuwekwa katika maeneo maalum.
130. Kufuatia kutangazwa kwa sehemu maalum, Mrakibu Mkuu wa polisi atateua kwenye eneo maalum idadi ya maafisa polisi saidizi na wenye cheo kama shughuli hiyo itakavyohitaji. [kifungu. 127]
Kuanzishwa na kudumishwa kwa vituo vya polisi katika sehemu maalum.
131. Inspekta Jenerali Mkuu atahakikisha kwamba kuna idadi ya kutosha ya vituo vya polisi vinaanzishwa na kudumishwa katika kila sehemu maalum ili watu waliokamatwa na maafisa wa polisi saidizi wanaweza kuletwa mbele ya Jeshi bila ya kuchelewa. [kifungu cha 128]
Sehemu maalumu kuhesabika kuwa moja katika mazingira fulani.
132. Iwapo sehemu zaidi ya moja ya sehemu maalum ni sehemu iliyotangazwa kutokana na maombi ya shughuli hiyohiyo, maeneo yote hayo maalum yatahesabika kuwa ni sehemu moja maalum kwa madhumuni ya utawala na usimamizi. [kifungu cha 129]
Utawala na usimamizi wa Jeshi la Polisi Saidizi.
133. Kulingana na maelekezo ya jumla ya Inspekta Jenerali Mkuu, utawala na usimamizi wa jeshi la polisi saidizi katika sehemu maalum utakuwa chini ya afisa polisi mwandaminzi aliyeteuliwa Inspekta Generali Mkuu kufuatia mapendekezo ya aliyeomba kutamkwa kwa eneo hilo. [kifungu cha 130]
Kuteuliwa kwa maafisa polisi saidizi
134. (1) Inspekta Jenerali Mkuu anaweza kuteua mtu yeyote anayefaa kuwa afisa polisi saidizi.
(2) Kufuatia uteuzi huo, afisa polisi huyo aliyeteuliwa atatamka yafuatayo mbele ya hakimu:–
55
"Mimi, .................................... wa ...................................... kwa dhati na kwa ukweli natamka na kuahidi kwamba nitakuwa mwaminifu na kuwa mkweli katika kuitumikia Jamhuri ya Muungano, na nitatii amri zote za maafisa wote nitakazopewa na kwangu mwenyewe zinazohusiana na Jeshi la Polisi Saidizi lililoko madarakani, na ambalo linaweza mara kwa mara kuwa madarakani, wakati wa utumishi wangu katika Jeshi hilo Saidizi la Polisi"
(3) Utawasililishwa kwa kila afisa polisi saidizi baada ya kufanya tamko hilo hapo juu mwongozo katika namna ifuatayo:-
SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI
Na. ...................................
Kwa………………............................................wa ……………………………..
Mimi, ....................................................., Kamishna wa polisi, kwa mujibu na kwa uwezo na mamlaka niliyopewa na Sheria ya Jeshi la Polisi Saidizi, nakuteua kuwa Afisa Polisi Saidizi wa eneo maalum la …………………….. wa daraja linaloendana na daraja la…………………….katika Jeshi la Polisi na ninatoa kwako mwongozo huu kukuidhinisha wewe kufanya kazi kama Afisa Polisi Saidizi.
Tarehe ..........................................
………………………………
Kamishna wa Polisi
(4) Baada ya kutoa tamko na baada ya kupokea mwongozo, mtu aliyeteuliwa atakuwa afisa polisi saidizi chini ya masharti ya Sheria hii.
[kifungu cha 131]
Kujiuzulu
135. (1) Afisa polisi saidizi hataweza kujiuzulu bila ya kupata kibali kwanza na kilichotolewa na afisa polisi mwandamizi msimamizi wa eneo maalum aliloteuliwa.
(2) Afisa polisi mwandamizi msimamizi wa eneo maalum anaweza kutokutoa kibali hicho kwa kipindi kisichozidi miezi miwili. [kifungu cha 13]
Kufutwa kwa mwongozo
136. (1) Mrakibu Mkuu anaweza kuondoa kutoka kwa afisa polisi yeyote saidizi mwongozo aliopewa chini ya kifungu cha 134 kama ameridhika kwamba:-
(a) afisa polisi saidizi hawezi kuwa au sio tena askari polisi saidizi hodari; au
(b) afisa polisi saidizi ameonekana na daktari aliyesajiliwa kutokuwa safi kiakili na kiafya kuendelea kutumikia zaidi; au
(c) afisa polisi saidizi ameamriwa kuondolewa kutoka katika jeshi la polisi saidizi chini ya kifungu cha 142; au
(d) afisa polisi saidizi amejiuzulu chini ya kifungu cha 135;
(e) kampuni inayomlipa afisa polisi saidizi haimhitaji afisa huyo kama afisa polisi saidizi.
(2) Baada ya kufutwa kwa mwongozo, afisa polisi saidizi atakoma
56
kuwa afisa polisi saidizi. [kifungu cha 133]
Malipo ya afisa polisi saidizi
137. (1) Kila afisa polisi saidizi aliyeteuliwa katika sehemu yoyote maalum atalipwa na kampuni ambayo iliomba kutangazwa kwa eneo maalum. Viwango vya malipo ya maafisa polisi saidizi isipokuwa maafisa polisi waandamizi vitapangwa kwa makubaliano na Inspekta Jenerali Mkuu.
(2) Kampuni hiyo itatoa kutoka katika malipo ya afisa polisi saidizi kiasi cha faini yoyote iliyotolewa kwa afisa polisi saidizi huyo chini ya kifungu cha 142 na itatumika katika namna iliyo sawa kama itakavyoweza.
[kifungu cha 134]
Vifaa
138. (1) Kila afisa polisi saidizi wakati wa kuteuliwa atapewa beji na namba . Beji hiyo litakuwa ni ushahidi wa ofisi wa afisa polisi huyo na katika muda wote atakuwa anatekeleza wajibu wake katika ofisi anatakiwa kuionesha beji hiyo.
(2) Kila afisa polisi atapatiwa na kampuni inayomlipa sare yenye usanifu ulioidhinishwa na Mrakibu Mkuu. Sare hiyo itatolewa kwa gharama za kampuni hiyo. [kifungu cha 135]
Uwezo, majukumu na kinga ya polisi saidizi.
139. (1) Kulingana na masharti ya Sehemu hii kila afisa polisi saidizi, ndani ya mipaka ya sehemu maalumu ambayo amechaguliwa, atakuwa na uwezo wa kukamata na kupekua kama walivyopewa wanajeshi wenye cheo kinacholingana na sheria yoyote kwa wakati inatumika na atatii amri zote halali za maafisa wake wa cheo cha juu na mahakimu.
(2) Kila afisa polisi saidizi atakuwa na haki ya kupata kinga zote alizopewa mwanajeshi yoyote chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote anapokuwa anatekeleza majukumu yak echini ya sheria hii.
(3) Kila afisa polisi ambaye wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Sehemu hii, anakamata mtu yeyote atampeleka bila kuchelewa katika kituo kilichopo karibu na eneo maalum ambalo amekamatwa na atamkabidhi kwa afisa wa Jeshi atakayemshughulika kutokana na sheria. [kifungu cha 136]
Makosa ya kinidhamu
140. Afisa polisi saidizi yeyote wa daraja la chini ya afisa polisi mwandamizi ambaye:-
(a) kwa makusudi hakutii amri halali; au
(b) anakataa au anazembea kutoa huduma au kutekeleza hati yoyote iliyoamriwa kihalali kutumikiwa au kutekelezwa naye; au
(c) amelewa wakati akiwa kazini; au
(d) hayupo kazini bila likizo; au
(e) ana hatia ya kitendo chochote, mwenendo, kutokutii amri au kuzembea kupelekea kuathiri amri nzuri na nidhamu,
Atahesabiwa kuwa ametenda kosa la kinidhamu na kosa hilo linaweza kupelelezwa kusikilizwa na kuamuliwa na mkosaji atawajibika kupata adhabu kwa mujibu wa na masharti ya Sehemu hii. [kifungu cha 137]
Uwezo wa
141. Afisa polisi saidizi anaweza kukamata au kuamuru kukamatwa kwa
57
kukamata kutokana na makosa
afisa polisi saidizi (ambaye sio afisa wa cheo chake au daraja la juu) ambaye ni mshtakiwa wa kosa chini ya kifungu cha 140; na afisa polisi saidizi yeyote anaweza, baada ya kupokea amri hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu, kumkamata bila ya hati na mara moja atamfikisha mbele ya afisa polisi saidizi aliyeamuru kukamatwa. [kifungu cha 138]
Adhabu ambazo zinaweza kutolewa
142. Afisa polisi mwandamizi anaweza kuchunguza kuhusu ukweli wa shtaka lolote chini ya kifungu cha 140 na kutoa uamuzi wake dhidi ya mtu aliyeshtakiwa, anaweza kutoa adhabu yoyote kwa mtu huyoe moja au zaidi kati ya zifuatazo:-
(a) karipio;
(b) faini isiyozidi malipo ya siku kumi;
(c) kushushwa kwa cheo au daraja;
(d) kufutwa kazini:
ilimradi kwamba hakuna amri ya kufutwa/kufukuzwa itakuwa na nguvu mpaka iidhinishwe na afisa polisi mwandamizi msimamizi wa eneo maalum. [kifungu cha 139]
Kuwasilishwa kwa beji, mwongozo na sare wakati wa kujiuzulu, nk.
143. (1) Pale ambapo afisa polisi sadizi amejiuzulu au amekoma kuwa na ofisi, mara moja atarudisha kwa afisa polisi mwandamizi msimamizi wa eneo maalum beji yake, mwongozo na vikorokoro vyote vya sare yake.
(2) Pale ambapo afisa polisi amefariki, mtu yeyote anayemiliki beji, mwongozo au vikorokoro vya sare alivyopatiwa chini ya Sheria hii, atawasilisha vifaa hivyo kwa afisa polisi mwandamizi msimamizi wa eneo maalum ambalo afisa polisi saidizi huyo alikuwa amepangwa ndani ya siku kumi na nne baada ya kifo hicho.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki afisa polisi saidizi atachukuliwa kuwa amejiuzulu siku ambayo kujiuzulu kwake kutoka Jeshi la Polisi Saidizi kumekuwa na nguvu chini ya Sehemu hii na atachukuliwa amekiuka kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki isipokuwa kama atafuata masharti ya kifungu hicho ndani ya siku moja baada ya kujiuzulu kwake kumekuwa na nguvu kama ilivyosemwa hapo juu. [kifungu cha 140]
Kurudishwa kwa beji, Mwongozo na sare zilizowasilishwa
144. Afisa sheria mwandamizi atalazimika, bila kuchelewa kupeleka kila beji na mwongozo aliopokea chini ya kifungu cha 143 kwa Inspekta Jenerali Mkuu. [kifungu cha. 141]
145. Kila mtu ambaye:-
(a) anakiuka masharti ya kifungu cha 143; au
(b) anamiliki begi, mwongozo au kikorokoro cha sare vilivyotolewa kwa matuminzi ya afisa polisi saidizi na hawezi kutoa sababu za kutosha kumiliki kwa vitu hivyo,
atakuwa na hatia ya kosa na atawajibika kutoa faini isiyozidi shilingi mia tano au kifungo cha kipindi kisichozidi mwezi mmoja au vyote.
[kifungu cha 142]
Afisa polisi saidizi
146. Afisa polisi saidizi atachukuliwa kuwa afisa kwa mujibu wa kifungu
58
atachukuliwa kuwa afisa kwa mujibu wa kifungu cha 243 chaa Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai
cha 243 chaa Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*.
[kifungu cha 143]
Mamlaka ya Jeshi la Polisi chini ya Sehemu hii kuwa nyongeza
147. Mamlaka yote aliyopewa na Sehemu hii Inspekta Jenerali Mkuu wa polisi na maafisa wengine wa Jeshi yatakuwa ni nyongeza katika mamlaka walionayo na sio katika kupunguza mamlaka mengine yoyote yaliyotolewa chini ya Sheria hii au Sheria nyingine yoyote na mamlaka hayo mengine yatatekelezwa katika namna sawa kama vile Sehemu hii haikuwa imetungwa
[kifungu cha 144]
SEHEMU YA KUMI NA SABA
MASHARTI MADOGO MADOGO
Kanuni G.N. No. 73 ya 1965
148. (1) Waziri anaweza kutengeneza kanuni zinazohusiana na yote au kati ya mambo yafuatayo:-
(a) uanzishwaji, utaratibu na usambazaji wa Jeshi, masharti ya uteuzi na utumishi, na vyeo, madaraja na teuzi mbalimbali zilizopo;
(b) wajibu unaotakiwa kufanywa na maafisa wa Jeshi, na mwongozo wao katika kutekeleza wajibu huo;
(c) malipo, marupurupu, viinua mgongo vya maafisa wa Jeshi;
(d) nidhamu na adhabu za maafisa wa Jeshi;
(e) maelezo na utoaji wa silaha, sare na mahitaji ya muhimu yakuwapatia wanachama wa Jeshi;
(f) masharti ya kustaafu,kujiuzulu, kufukuzwa, kuondolewa, kushushwa cheo au kugeuzwa kwa wanachama wa Jeshi;
(g) masharti ya likizo ya Jeshi;
(h) maombi na utawala wa Mfuko wa Tuzo wa Polisi
(i) utoaji wa beji za tabia njema na malipo ya utendaji mzuri na utozwaji kikombozi wa vitu hivi;
(j) mambo yote yanayotakiwa na Sheria hii kufafanuliwa au kuelezwa na kanuni;
(k) kiujumla kwa amri bora na serikali ya Jeshi
(2) Waziri anaweza kutengeneza kanuni kwa ajili ya uongozi/ utawala kwa jumla wa afisa polisi wa daraja la chini maalum na, bila kuathiri ujumla wa mamlaka hayo, anaweza kutengeneza kanuni kuhusiana na:-
(a) uteuzi wao, kuustaafu, kuondolewa na kufukuzwa;
(b) vyeo na ujira wao;
(c) masharti yao ya utumishi na nidhamu;
(d) mafunzo yao;
(e) wajibu na majukumu yao wakati wakiwa kazini;
(f) sare na vifaa vya kuvaliwa na silaha watakazobeba;
(g) matumizi ya Sehemu ya KWANZA mpaka KUMI NA NNE ya Sheria hii.
59
(3) Rais anaweza kutengeneza kanuni chini ya Sehemu ya KUMI NA SITA:-
(a) kufafanua kitu chochote ambacho kinatakiwa au kinaweza kufafanuliwa;
(b) kufafanua mafunzo polisi saidizi;
(c) kwa ujumla utekelezaji mzuri wa madhumuni na masharti ya Sehemu hiyo. [kifungu. 145]
Imefutwa kwa R.L. Sura ya 55 na 59 Sheria Na. 22 ya 1955 kifungu cha 14
149. [Inafuta Sheria ya Jeshi la Polisi * na Sheria ya Alama za Vidole*.]
[kifungu cha 146]
60
JEDWALI LA KWANZA
FOMU I
FOMU YA KUTAMKA UANDIKISHWAJI TANZANIA
SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI
(Kifungu cha 15)
Mimi, ....................................., kwa dhati na kwa ukweli mtupu natamka kwamba nitakuwa mwaminifu na kuwa na utii katika Jamhuri ya Muungano, na kwamba nitatumikia kwa uaminifu katika kipindi chote cha utumishi wangu katika Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano na nitatii amri zote za Rais na za maafisa walio juu yangu, na nitajihusisha mwenyewe na yote yanayohusiana na Jeshi ambayo yanatumika au ambayo mara kwa mara yatakuwa yanatumika.
................ ...................................
(Sahihi au alama ya Afisa Polisi)
Imetamkwa leo hapa tarehe ............................, mwezi wa......................... Mwaka 20.....................
Mbele yangu......................................................................................
(Sahihi ya Hakimu au Afisa)
FOMU 2
UTEUZI WA MAAFISA POLISI MAALUM WA TANZANIA.
SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI)
(kifungu cha 81)
Kwa ...................................., wa.................... Mimi, niliyesaini hapo chini ...................., kwa mamlaka niliyopewa na Sehemu ya XII ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi nakuteua wewe kuwa afisa polisi maalum kuanzia ..................... mpaka kwa taarifa zaidi.
Imeandikwa leo tarehe.................... Mwezi ....................................., 20..................
Imesainiwa......................................................
61
FOMU YA 3
TAARIFA KWA AJILI YA KUSIMAMISHA AU KUAMUA UTEUZI WA AFISA POLISI MAALUM WA TANZANIA
SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI)
(Kifungu cha 82)
Futa sehemu isiyotakiwa
Kwa ...................................., wa............... Mimi, niliyesaini hapo chini ...................., kwa mamlaka niliyopewa na Sehemu ya Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi nakupa taarifa kwamba uteuzi wako kama afisa polisi maalum kwa ajili ya ................................., Mimi,Wilaya, Mkoa, kama itakavyokuwa, uliofanyika, imeandikwa kwa leo tarehe ..........., mwezi wa…………20........, umesimamishwa (au kuamuliwa, kama itakavyoweza kuwa kuanzia tarehe iliyoonyeshwa.
Imeandikwa tarehe leo ....................... Mwezi wa ...................., 20........
JEDWALI LA PILI
FOMU YA 4
VIWANGO VYA MALIPO YA KUONDOLEWA
SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI)
(Kifungu cha 23)
(I) Shilingi mia mbili wakati wa mwaka wa kwanza wa utumishi; shilingi mia na hamsini wakati wa mwaka wa pili wa utumishi; shilingi mia moja wakati wa mwaka wa tatu wa utumishi au mwaka mwingine wowote wa utumishi unaofuata.
(II) Iwapo ni afisa polisi mwanafunzi aliyeorodheshwa chini ya kifungu cha 14(2) ya Sheria hii, shilingi arobaini katika kipindi cha mwaka wa kwanza cha utumishi wake; shilingi sabini katika kipindi cha mwaka wa pili cha utumishi wake; na shilingi mia moja katika kipindi cha mwaka wa tatu au mwaka wowote unaofuata kama afisa polisi mwanafunzi.
62
JEDWALI LA TATU
FOMU YA TAMKO LA WALIOORODHESHWA
(Kifungu cha 111)
Mimi, ....................................., kwa dhati na kwa ukweli mtupu natamka kwamba nitakuwa mwaminifu na kuwa na utii katika Jamhuri ya Muungano, na kwamba nitatumikia kwa uaminifu katika kipindi chote cha utumishi wangu katika Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano na nitatii amri zote za Rais na za maafisa walio juu yangu, na nitategemea sheria zote zinazohusiana na Jeshi la Polisi la Akiba zinazotumika au ambazo mara kwa mara zinaweza kutumika.
Saini au Alama ya Mtunza Akiba............................................
Imetamkwa hapa ......................, mbele yangu …………............ leo tarehe .................., 20........, na ............... baada ya kumuelezea yote kuhusu kanuni na masharti ya kujiunga kwake katika Jeshi la Polisi la Akiba, na ameonekana kuelewa kila kitu.
Sahihi ya kuthibitisha Afisa Polisi au Hakimu................................................................

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni